Klabu ya Yanga imetangaza mabadiliko ya tarehe ya mkutano mkuu wa wanachama ambapo sasa umepangwa kufanyika Juni 10, mwaka huu
Awali mkutano huo, ulipangwa kufanyika Juni 17, lakini sasa mabadiriko hayo yanaurudisha nyuma kwa wiki moja
Akiongea na mwandishi wa tovuti ya Kandanda Katibu wa matawi ya Yanga, Boaz Kifukwe, alithibitisha kuwepo kwa mabadiriko hayo
Aidha Katibu huyo, alielezea sababu za mabadiriko za hayo “Tunataka twende na wakati ligi inaisha kesho, hivyo tunataka tuanze maandalizi ya msimu ujao pamoja na kuindaa timu na michuano ya kimataifa”
Akielezea baadhi ya Ajenda za mkutano huo Katibu huyo alisema “ni Ajenda za mkutano mkuu wa katiba ikiwa ni kupitia mapato na matumizi na kupitia yatokanayo na mkutano uliopita” alisema Kifukwe
Pia Katibu huyo alifafanua kuwa, suala la mabadiliko ya mfumo uendeshaji wa klabu linaweza likajadiriwa katika mkutano ikiwa ni sehemu ya mengineyo
Katibu huyo amewataka Wanachama kulipia kadi zao ili kuruhusiwa kushiriki katika mkutano huo kwa mujibu wa Katiba ya klabu ya klabu hiyo
Aidha katika mkutano huo kadi zote mpya (za benki ya posta) na zile za zamani (za kitabu) zitatumika jambo la kuzingatiwa lazima ziwe zimelipiwa.