Kaimu katibu mkuu wa Yanga SC, Omary Kaya amenukuliwa kwamba Shirikisho la soka nchini (TFF) ndiyo wanaoweza kuzungumza kuhusu kufungiwa kwa kiungo wao Mohamed Issa ‘Banka‘ Mara baada ya tovuti hii (kandanda.co.tz) kuhoji kwanini Banka hajaanza kuitumikia Yanga iliyomsajili katika usajili uliofungwa hivi karibuni.
Mengi yamekuwa yakisemwa kuhusu mchezaji huyo wa timu ya Taifa ya Zanzibar- ikiwemo taarifa kuwa mchezaji huyo wazamani wa Mtibwa Sugar FC amefungiwa mwaka mmoja na Shirikisho la soka Afrika ( Caf) kufuatia kufeli kwa vipimo vilivyofanyika November mwaka jana katika Cecafa Senior Challenge Cup huko Kenya.
Kaimu Katibu Mkuu ameongeza kuwa klabu yake bado haijapata taarifa yoyote rasmi kuhusu kufungiwa au kutokufungiwa kwa mchezaji wao mpya Mohamed Issa Banka, kutoka TFF. Wao pia wanasubiria taarifa hiyo.
Lakini pia inawezekana klabu ya Yanga ilimsaini Banka kabla ya barua ya kufungiwa kutumwa TFF (Kama barua ipo), hivyo wakati wakipeleka taarifa ya wachezaji wa msimu huu ndipo labda walipogundua kimyakimya kuwa hawataweza mtumia mchezaji huyo.
Muda ni jibu la kila kitu, tutajaribu kutafuta ukweli zaidi kutoka kwa Banka na wahusika zaidi.