Sambaza....

KIKOSI cha mabingwa wa soka Tanzania Yanga Sc, kinatarajia kusafiri kesho asubuhi kueleka Shelisheli tayari wa mchezo wa marejeano wa michuano ya vilabu bingwa Afrika dhidi ya wenyeji wao St Louis Fc, mchezo ubaotaji kupigwa jumatano ijayo kunako dimba la Stade Liete.

Muda mfupi uliopita Ofisa habari wa Yanga, Dismas Ten, aliielezea safari hiyo kuwa jumla ya nyota 20 na viongozi 10 kati yao 8 kutoka benchi la ufundi watasafiri asubuhi ya kesho kupitia Nairobi tayari kwa mchezo huo muhimu siku ya jumatano.

“Maandalizi yote muhimu tumeyafanya, na timu imefanya mazoezi ya mwisho leo tayari kwa safari kwenye kikosi bado wataendelea kukosekana wachezaji kama Amis Tambwe, Donald Ngoma, Abdalla Shaibu na kinda Yohana Mkomola, hii ni kwa sababu bado wanauguza majeraha yao

Akieleza zaidi Ten alisema kuwa, kiungo Thabani Kamusoko ambaye amepona majeraha yake hivi karibuni na kuanza mazoezi mepesi pia ameondolewa kwenye orodha ya nyota ambao wangesafiri kueleka Shelisheli ili apate muda wa kujifua zaidi ili kurejesha makali yake, pia mshambuliaji Obrey Chirwa naye hayumo kwenye orodha ya wachezaji watakaosafiri kwa sababu ya maumivu ya misuli aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Majiamaji.

 

“Ilikuwa asafiri kueleka Shelisheli, lakini imelazimu benchi la ufundi kumuondoa kwa sababu bado haakuwa sawasawa kwa 100%, hivyo anahitaji muda wa kujifua zaidi ili kupata utimamu wa mwili tayari kwa mapambano uwanjani, daktari wake pia amethibitisha kuwa mchezaji anatakiwa apate muda wa kujiweka sawa kabla hajaanza kucheza mechi kulingana na majeraha aliyokuwa nayo” alisema ofsa habari huyo asiye na maneno mengi

Orodha kamili ya wachezaji wanataraji kuwemo kwenye safari hiyo ni pamoja na magolikipa

Ramadhani Kabwili, Beno Kakolanya,Youthe Rostand

Walinzi ni

Hassan Kessy,Juma Abdul,Mwinyi Haji,Gadiel Michael,Nadir Haroub,Patto Ngonyani,Kelvin Yondani,Said Juma

Viungo ni

Papy Tshishimbi,Pius Buswita,Raphael Daud,Yussuf Mhilu,Ibrahim Ajib,Said Mussa,Emmanuel Martin,Geoffrey Mwashiuya,Juma Mahadhi,Emmanuel Martini.

Sambaza....