Sambaza....

Yanga wapo katika hatua nzuri ya kumalizana na mshambuliaji wa Al Hilal Makabi Lilepo. Kuachwa kwa Benard Morrison kunapelekea kuipa nafasi Yanga kumuongeza Lilepo ambae anapokea mshahara mkubwa na Al Hilal. [Mwanaspoti]

Mbali na Lilepo, Yanga pia inataka kurudi kwa rafiki zao Union Maniema kumchukua winga mwingine wa kulia Maxi Mpia Nzengeli. [Mwanaspoti]

Ni rasmi Yanga ilipokea milioni 200 kutoka kwa Azam Fc katika mauzo ya Feisal Salum, kupitia mkutano mkuu kwenye mapato na matumizi inaonyesha Yanga imepata milioni 200 katika mauzo ya wachezani na ni mchezaji mmoja pekee Yanga wamemuuza msimu huu. 

Feisal Salum akitambulishwa rasmi na Azam Fc.

Kocha mpya wa Yanga Miguel Angel ameshinda kikombe kimoja pekee akiwa kama kocha mkuu. Ameshinda kombe la FA nchini Morocco akiwa na klabu ya Hassania mwaka 2019.

Klabu ya Simba ipo katika mazungumzo ya kumsajili mlinda mlango Caiques Luis Santos ambae aliidakia timu ya Taifa ya Brazil U-20 na kwasasa anaitumikia timu ya Seria C Ypiranga-SC nchini Brazil. [Nuhu Adams]

Bruno Gomes ameongeza miaka miwili kuendelea kuitumikia Singida Fountaine Gate na kuzima uvumi wa kuelekea timu za Kariakoo ambapo wote Simba na Yanga wamekua wakitajwa kumuhitaji Mbrazil huyo.

Bruno Gomes.

Manchester City wanafikiria kuwasilisha ombi la kumnunua beki wa kulia wa Paris St-Germain Achraf Hakimi, 24, na “haitasita” kulipa ada kubwa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Morocco. [Marca]

Liverpool, Manchester United na Chelsea watafanya mikutano na maajenti wa mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, wiki ijayo kuhusu uwezekano wa kuhamia Ligi ya Premia. [Express]

Mabingwa hao wa Lgi Kuu Qatarm inaelezwa wapo tayari kumfanya mshambuliaji huyo ambaye alikuwa akichezea Al Qadsiah FC ya Ligi Daraja la Kwanza Saudi Arabia kuwa mopja ya wachezaji ghali kwenye kikosi hicho[Mwanaspoti]

 

 

 

Sambaza....