Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa mtendaji wake mkuu Senzo Mazingiza umekiri kupokea ofa za vilabu vikubwa Barani Afrika wakihitaji huduma ya mshambuliaji wao Fiston Mayele.
“Kwa hakika, nimekuwa nikipokea simu – unajua, nina watu nimefanya nao kazi kote Afrika. Nimepokea simu tatu kutoka Afrika Kusini, vilabu vikubwa vinavyoonyesha nia,” Mazingiza aliiambia SABC Sport.
Licha ya kukiri Yanga haijapokea ofa rasmi kwa maandishi lakini mtendaji huyo wa Yanga ameweka wazi hawapo tayari kusikiliza ofa yoyote kwa mshambuliaji wao huyo mwenye mabao 16 mpaka sasa.
“Ingawa nia haijaonyeshwa kwa maandishi au kitu kama hicho, maswali yamekuwepo na nimekuwa wazi kusema kwamba hapatikani, ana mkataba nasi na tunataka kufanya vizuri kwenye mashindano ya vilabu. [Caf Champions League].” Senzo Mazingisa.
Vilabu viwili vya Soweto Orlando Pirates na Kaizer Chiefs vimetajwa kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo kutoka Congo na mchezaji wa zamani wa AS Vita.
Mara mbili mfululizo vilabu hivyo vimefanikiwa kuitoa Simba katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Afrika.