Wananchi Yanga wapo katika hatua nzuri ya kwenda kuweka historia katika soka la Afrika wakielekea katika mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United
Mpaka sasa Yanga wana faidi ya ushindi wa mabao mawili kwa sifuri nasasa wanarudi kucheza nyumbani Benjamin Mkapa na afisa habari wa klabu ya Yanga Alli Kamwe kuelekea mchezo huo wa marudiano amesema “Jumapili tuna mchezo muhimu na wakihistoria katika klabu hii ni mchezo wetu wa pili wa robo fainali dhidi ya River United, kwahiyo niwaombe wapenzi, mashabiki kujitokeza kwa wingi siku ya jumapili na kuwapa nguvu wachezaji wetu.”
Alli Kamwe pia amewasisita watu kununua tiketi mapema kuelekea mchezo huo ili wajae kwa wingi kiwanjani na kuwaachia deni wachezaji wao na kuwataka wote watakaokwenda kiwanjani kuvaa jezi za kijani na njano za Yanga.
“Namna nzuri ya kuhamasisha wachezaji na viongozi wetu ni kununua tiketi mapema, uwanja ukijaa mapema hata wachezaji wanapata morali, kwahiyo nawaombeni Wanachi tukate tiketi mapema ili tukaweke historia pamoja,” alisema na kuongeza
“Mtoko wetu wa Jumapili ni wa Kivumbi na Jasho na tunataka tuwe na Dress Code maalum, tunataka Uwanja wa Mkapa jumapili hii uwe wa njano na kijani, Jezi za yanga zipo katika duka letu hapa makao makuu ya klabu, mje mzinunue.” Alli Kamwe.
Yanga wanaikaribisha Rivers United wakiwa mguu mmoja kwenda nusu fainali kwani wana mtaji wa mabao mawili aliyoyafunga Fiston Mayele katika mchezo wa awali ugenini nchini Nigeria.