Sambaza....

Kwa mujibu wa taratibu za shirikisho la mpira wa miguu barani Africa , CAF nchi 12 zenye ligi bora hutoa timu 4 kwenye mashindano ya vilabu ya CAF , yani ligi ya mabingwa barani Africa pamoja na kombe la shirikisho barani Africa.

Msimu wa mwaka 2019/2020 Tanzania ilifanikiwa kuwa kwenye nchi 12 zenye ligi bora barani Africa na ikatoa wawakilishi wanne kwenye michuano ya kimataifa ya CAF.

Simba na Yanga zilituwakilisha kwenye ligi ya mabingwa barani Africa huku KMC FC pamoja na Azam FC zilituwakilisha kwenye kombe la shirikisho barani Africa.

Gerson Fraga akimthibiti Bruce Kangwa wa Azam fc

Kwa bahati mbaya timu zetu zilifanya vibaya kwenye mashindano hayo ya kimataifa ya CAF. Kufanya kwao vibaya kukaiweka ligi yetu kushika nafasi ya 13 kwenye orodha ya ligi bora Africa.

Ligi kuu ya Libya ilishika nafasi ya 12 baada ya klabu ya Al Nasr kufika hatua ya robo fainali kwenye michuano ya kimataifa ya CAF. Hivo Libya ikawa na nafasi ya kutoa timu 4 msimu ujao.

Jana shirikisho la soka barani Africa lilitoa hukumu ya kuifungia Libya kutoshiriki michuano ya CAF msimu ujao kutokana na Libya kushindwa kumaliza ligi.

Swali kubwa hapa linabaki Tanzania itapata tena nafasi ya kupeleka timu 4 kwenye michuano ya kimataifa ya CAF kutokana na Libya kufungiwa ? Libya iko nafasi ya 12 na Tanzania iko nafasi ya 13.

Sambaza....