
Klabu ya Yanga imesema kuwa, itakuwa imeshamilisha uwanja wake mmoja wa mazoezi hadi itakapofika Desemba mwaka huu.
- AFCON 2027: Tanzania Inajiandaa – Kandanda.co.tz Yaleta Maeneo Muhimu ya Mashindano!
- Pamoja AFCON 2027
- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo Dismas ten. Ten amesema kuwa mpango wa klabu ni kuwa na viwanja viwili, kimoja cha nyasi asili na kingine cha nyasi bandia ambavyo vitakidhi mahitaji ya klabu.
“Tuna eneo kubwa.. tunaweza kuweka viwanja viwili… kwa sasa uongozi unajitahidi kuhakikisha eneo hili linakamilika ili liwe tayari kuchezewa”
Yanga hutumia zaidi ya Milioni 36 kwa ajili ya kulipia viwanja vya mazoezi, hivyo uongozi wa klabu hiyo unaona kuharakisha kuwa na uwanja wake kutaokoa Mamilioni hayo.
“Uongozi upo makini kuhakikisha eneo hili linakuwa tayari kimatumizi ifikapo mwezi desemba mwaka huu..” alielezea Ten
Hadi sasa, inakadiliwa kuwa zoezi la kusawazisha
eneo hilo limefikia 80% kukamilika huku klabu ikiwa na mipango mikubwa zaidi
hasa kulizunguushia ukuta au majukwaa baada ya eneo hilo kukamilika kwa 100%.