Baada ya sare ya bila kufungana baina ya Simba sc na Azam fc jana sasa leo ni zamu ya Yanga sc na Ruvu Shooting ya Masau Bwire katika dimba la Uhuru jijini Dar es salaam katika mwendelezo wa Ligi Kuu Bara.
Baada ya sare ya jana sasa Simba imefikisha alama 82 huku Yanga wao wakiwa na alama 80. Hivyo ushindi wowote leo watakaoupata Yanga dhidi ya Ruvu Shooting utawarudisha kileleni kwani watafikisha alama 83 moja zaidi ya Simba sc.
Kueekea mchezo huo tayari pande zote mbili zimejinasibu kufanya vizuri na kuzoa point tatu mbele ya mwenzake. Ikumbukwe Yanga wapo katika mbio za kutaka ubingwa huku Ruvu Shooting wao wakiwa kwenye vita ya kujinasua isiteremke daraja.