Timu ya Yanga imeyaaga mashindano ya Azamsports FederationCup baada ya kutolewa na Singida Utd kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja katika dakika 90 za mchezo.
Mchezo huo wa mwisho wa robo fainali uliopigwa Katika dimba la Namfua, Sasa unaifanya Yanga kutolewa na Kuungana na wenzao Azam Mji, Njombe na Prisons kuyaaga mashindano.
Yanga walikua wakwanza kupata bao ambapo Katika dakika ya 23 Yusuph Mhilu aliiandikia bao Yanga kwa kuunganisha kona safi iliyopigwa na Ajib Migomba. Mpaka mapumziko Yanga ilikua inaongoza kwa goli hilo moja.
Kipindi cha pili Singida Utd walirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata goli mapema tuu lililowekwa kambani na kiungo wake Kenny Ally baada ya kupokea pasi safi ya Mudathiri Yahya.
Mpaka mchezo unamalizika dakika 90 Singida Utd 1 Yanga SC 1, hivyo kufanya mchezo uende katika hatua ya kupigiana penalty. Ambapo Singida Utd walipata penati nne na kukosa moja huku Yanga walipata penati mbili na kukosa mbili na kuifanya Singida Utd kuungana na JKT Tanzânia, Stand Utd na Mtibwa Sugar nusu fainali.
Kwa upande wa Yanga waliopata penati ni Kelvin Yondani na Gadiel Michael huku Pappy Tshishimbi akipaisha na Emmanuel Martin penati yake kugonga mwamba.
Kwa Singida Utd wachezaji Rusheshangoga, Kenny Ally na Eliswenye Sumbi “Msingida” akipiga penati ya ushindi, huku beki Malik Ntiri akikosa penati!
Singida Utd sasa itavaana na JKT Tanzânia Katika mchezo wa nusu fainali utakaopangiwa tarehe hapo baadae.