Moja ya kauli ambazo Afisa Habari na mhamasishaji wa Yanga , Antonio Nugaz anazozikuza ni Yanga kuwa na uwezo wa kuifunga Pyramid FC goli 3-0 katika uwanja wa CCM KIRUMBA. Hakuna kinachoshindikana lakini kiuhalisia ni ngumu kwa Yanga kuifunga Pyramid FC 3-0 . Kwanini nasema hivo ?
RECORD NZURI YA PYRAMID UGENINI
Pyramid FC msimu huu amekuwa na akifanya vizuri katika mechi za ugenini . Katika mechi kumi na mbili (12) zilizopita amecheza mechi nne (4) za ugenini na amefanikiwa kushinda mechi tatu (3) na kufungwa mechi moja peke yake tena dhidi ya Zamaleki FC miamba mikubwa ya soka barani Afrika, na Zamaleki. Wakati Zamaleki wakiifunga Pyramid FC, Ahly walifungwa nyumbani kwao na PYRAMID FC. Kwa hiyo Pyramid FC wamekuwa wazuri hata kwenye viwanja vya ugenini. Hapa ndipo ugumu wa Yanga kuifunga Pyramid FC goli 3-0 unapoanzia.
WASTANI MZURI WA MAGOLI YA KUFUNGWA
Katika mechi kumi na mbili (12) zilizopita Pyramid FC wamefungwa magoli kumi (10) ikiwa ni wastani wa kufungwa goli 0.8 kwenye kila mechi ambayo wameingia uwanjani. Hii inadhihirisha ukuta wao ni mgumu sana. Na katika mechi ambazo wamefungwa ni mechi tatu tu ambazo wameruhusu magoli mawili na zaidi, dhidi ya Zamaleki walipofungwa 3-0 ugenini , waliruhusu magoli mawili mawili kwenye hizi mechi mbili dhidi ya Eltangy mechi iliyoisha kwa Pyramid FC kushinda 3-2 na Elgaesh mechi iliyomalizika kwa Pyramid FC kutoka sare ya 2-2. Na katika mechi 12 zilizopita , Pyramid FC walifanikiwa kupata clean sheet katika mechi 6. Wana asilimia 50 ya kupata Clean sheet kila wanapoingia uwanjani.
WASTANI WA KAWAIDA WA SAFU YA ULINZI NA USHAMBULIAJI YA YANGA
Yanga imecheza mechi nane (8) mpaka sasa hivi na katika hizo mechi nane (8 ) amefanikiwa kufunga magoli nane (8) na kufungwa magoli nane (8) pia. Hii ina maana ya kwamba Yanga ina wastani wa kufunga goli moja kwenye kila mechi. Hivo safu yao ya ushambuliaji haina uwezo wa kufunga goli 3 kama wanavyojinadi wana Yanga. Pia safu yao ya ulinzi haina uwezo wa kutoruhusu goli kwa sababu ina wastani wa kuruhusu goli moja kwenye kila mechi. Hivo inatia mashaka kwa Yanga kuwa na uwezo wa kutoruhusu waarabu wasipate goli tena ikizingatiwa kwenye mechi zilizopita za kimataifa Yanga aliruhusu goli kwenye mechi za ugenini, Rollers walipata goli na Zesco walipata goli kwenye uwanja wa nyumbani wa Yanga.
MATOKEO YA YANGA MSIMU HUU
VPL
YANGA vs RUVU SHOOTING (0 – 1)
YANGA VS PLS TZ (3-3)
YANGA VS COAST (1-0)
MBAO VS YANGA (0-1)
CAF CL
YANGA VS ROLLERS (1-1)
ROLLERS VS YANGA (0-1)
YANGA VS ZESCO (1-1)
ZESCO VS YANGA (2-1)