Sambaza....

Jana Ligi Kuu Bara iliendelea katika dimba la uwanja wa Taifa ambapo Yanga waliikaribisha Lipuli fc  “Wanapaluhengo”. Yanga waliweza kutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani na kuweza kupata ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Achana na utata wa waamuzi katika mchezo ule haswa pale mpira alioudaka kipa Metacha Mnata ukileta kizaazaa kama ni kona au ulipita katika mstari wa goli, tazama jinsi Lipuli fc ilivyobadilika kiuchezaji na kuweza kuithibiti Yanga haswa katika kipindi cha pili.

Kwa namna ya pekee kabisa tumpongeze kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Lipuli ndugu Julio Eliezer kwa kuonesha ukomavu wa juu kabisa kwa kubadili mfumo wa Lipuli kucheza soka la kisasa kwenye mechi dhidi ya Yanga.  Pasipo kujali matokeo maana kipindi cha pili Yanga walizidiwa sana.

Julio alifanikiwa kuisoma Yanga na kuweza kubadili mfumo wa timu yake hivyo aliwashika Yanga vizuri, hakika huyu ni hazina ya Lipuli. Lipuli msihangaike na makocha wengine wowote labda apewe msaidizi tu yeye aendelee kuwa kocha mkuu.

Kumbukeni huyu kocha  ni mtu makini sana na kawasumbua makocha nguli wa Tanzania kama Richard Adolf wa Tanzania  Prison, lakini kwa Julio kamvulia kofia na kwenda kumpa saluti hiyo ni heshima kubwa kwa Lipuli, mkoa Iringa na Julio mwenyewe.

Hongera Wanapaluhengo mtafakari huyu Julio kwa kina. Hivi viongozi mngekuwa mmetatua matatizo ya timu nadhani Yanga alikuwa anakufa pale kwa Mkapa lakini pamoja na matatizo Julio kajitahidi sana kuiamsha na timu na kunyanyua viwango vya wachezaji.

Sambaza....