Sambaza....

Baada ya matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili katika mchezo wa Simba na Yanga uliopigwa January 4 katika dimba la Taifa limeacha mengi nyuma yake haswa kwa upande wa Simba

Si kwa wachezaji tu bali hata viongozi na mashabiki walitoka uwanjani wakiwa wanyonge baada ya sare ile, huku ikionekana kama Simba imepoteza mchezo. Na hii ni kutokana na “Comeback” ya nguvu ya Yanga ya kufunga magoli mawili ndani ya dakika 5 na hivyo kufuta uongozi wa mabao mawili ya Meddie Kagere na Deo

Mzamiru Yasin akimdhibiti Haruna Niyonzima

Goli la kwanza la Yanga lilifungwa na Balama Mapinduzi baada ya kuupitia mpira katika miguu ya Mzamiru Yasin  la kuachia fataki lililomshinda Aishi Manula.

Baada ya sare ile mpaka leo haijulikani alipo “kiungo punda” Mzamiru Yassin. Akiwa hajaonekana katika michezo yote minne ya Ligi Kuu Bara na mchezo mmoja wa FA dhidi ya Mwadui fc.

Balama Mapinduzi akipiga shuli lilizoo goli baada ya kumpokonya mpira Mzamiru Yassin

Katika mchezo huo Mzamiru alianza katika eneo la kiungo sambamba na Jonas Mkude huku juu yao akiwa Cleotus Chama kama namba 10.

Je makosa ya kusababisha goli katika mchezo ule ndio yamemfanya kukosa nafasi katika kikosi cha Wekundu hao?  Au kuna sababu nyingine za kiufundi au ni majeruhi ndio zinafanya Mzamiru asionekane uwanjani mpaka sasa akiwa na jezi ya Simba!?

Sambaza....