Sambaza....

Katikati ya Mvuto na hamasa kuna mstari ambao mpaka sasa unaitenganisha Yanga, klabu kubwa hapa nchini. Hawa ndiyo wanajiita wananchi, wananchi wawekezaji wa klabu yao. Uwekezaji ambao mpaka sasa hivi umekuwa karibu na ndimi zao na kuwa mbali na vitendo vyao.

Vitendo vyao vinakuwa tofauti kabisa na maneno ambayo wanaongea kila siku. Inawezekana kabisa imani yao iko katika uwekezaji wa klabu, lakini hakuna mazingira ambayo wametengenezewa kuwa wawekezaji.

Ulitazama Simba Day? Na unalikumbuka tamasha la wiki ya wananchi ?, matamasha mawili ambayo yalikuja na hitimisho kuwa mashabiki wa Simba ndiyo wawekezaji wa klabu yao.


Simba hawakutumia na viingilio vikubwa kiasi hiki, angalau kama tulikuwa na lengo la kuujaza uwanja tungeweka shilingi 2,000 au 3,000 lakini si 5,000 kamanda” Ally Hassan, shabiki wa Yanga alipohojiwa na Kandanda.


Siyo mashabiki wa Yanga. Mashabiki wa Simba wanaijali sana timu yao kuzidi mashabiki wa Yanga. Wanaipenda kupitiliza timu yao kuzidi wa Yanga.

Mashabiki wa Simba ndiyo wanaojua nini maana ya kuwekeza. Hawa ndiyo wamejiwekea mazingira ya kuwekeza ndani ya klabu yao.

Wananunua sana jezi kuzidi mashabiki wa Yanga, ndiyo maana sikushangaa niliposikia jezi elfu 20 zilizotengenezwa kwa ajili ya Simba Day zimeisha.


Nani anaweza kuisaidia Yanga kuleta Hamasa nje ya Uwanja?

  • Twalibu Abdallah (Mtangazaji wa EFM)
  • Said Kilumanga (Mtangazaji Channel Ten)
  • Maulid Kitenge (Mtangazaji EFM)

Tetesi tulizozipata, kati ya hawa mmojawapo anaweza kuja kuwa msemaji wa klabu.


Mashabiki wa Simba wanajivunia sana kuvaa jezi za timu yao, wanajivunia sana ngozi zao kuzivika kwa vazi jekundu.

Hawa ndiyo wawekezaji, wawekezaji ambao wanajua majukumu yao sahihi. Wawekezaji ambao wanajua kujaza uwanja ni kuwapa hamasa wachezaji.

Tofauti kabisa na Yanga. Ulishuhudia mechi dhidi ya Township Rollers jana? Uliona idadi ya mashabiki wa Yanga waliokuja kuishangilia timu yao?

Huwezi kujiita mwekezaji wakati hutaki kuwekeza hata kwenye hamasa ya mashabiki. Wachezaji huitaji hamasha ili kujituma zaidi.

Hiki kinakosekana kwa Yanga. Na hapa ndipo tunaporudi kwenye mstari unaotenganisha mvuto na hamasa. Kwa sasa Yanga inakosa vyote ndiyo maana inahangaika sana.

Matukio katika picha: Yanga SC 1 -1 Towship Rollers


-Patrick Sibomana akipasha misuli kabla ya mechi

-Wachezaji wa Yanga wakipasha misuli kabla ya mechi kuanza.

-Wachezaji wakisalimiana kabla ya mchezo kuanza

-Heka heka upande wa pembeni wakati wa kipindi cha kwanza

-Nahodha wa Yanga, Papy Tshishimbi akionyesha matumizi ya kitambaa alichovaa mkononi

-Tshishimbi akiuliza “Mbona Balama umesimama tu hapo, tafuta nafasi nikupe”

-“Kama hamfunguki basi naendele kuuchezea hapa hapa” Tshishimbi

-Mohamed Issa “Nipe mimi kama Balama hafunguki”

-Balama “Jamani si nipo hapa, huyu Makilikili haniwezi wewe nipe tu”

-Balama akipambana

-Metacha “Paul umezingua, mnamuachaje anadrible vile, dahh mnaniharibia” , Paul “We nawe urefu haukusaidii kuziba goli…daahh” Hii ni baada ya Yanga kufungwa goli la kwanza.

Mashabiki wa Yanga waliojitokeza uwanjani.

Sambaza....