Jana kulikuwa na mechi ya ligi kuu Kati ya Yanga na Prisons , mechi ambayo ilihudhuliwa na mtandao wa kandanda.co.tz katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Baada ya mechi ile mtandao huu ulifanya mahojiano na Afisa Mhamasishaji wa klabu ya Yanga ndugu Antonio Nugaz kuhusiana na mchezo huo wa jana ambao mashabiki wengi walikuwa hawana furaha .
Alipoulizwa kuhusu kukosa furaha mashabiki wa Yanga baada ya mchezo huo Antonio Nugaz alidai kuwa lazima wakose furaha kwa sababu wanagharamika.
“Lazima wakose furaha kwa sababu unakuta wao ndiyo wanatumia gharama kuja uwanjani kwa ajili ya kuangalia mpira , wanajibana kwa vingi .
“Unakuta shabiki anapanda daladala kwa nauli ambayo amejibana ili aje uwanjani , anajinyima mpaka hela ya kula ili apate hela ya kiingilio uwanjani , lazima aumie “alisema Afisa Mhamasishaji huyo wa Yanga.
Kuhusu mashabiki kulalamika timu kutoshinda mechi ya pili mfululizo dhidi ya Mbeya City na Prisons , Antonio Nugaz amedai kuwa Yanga haichezi Rede
.
” Timu yetu haichezi Rede eti kila siku ishinde , tunacheza mpira wa miguu na mpira wa miguu una matokeo matatu kufungwa , kushinda na kutoka sare”alimalizia Antonio Nugaz