Sambaza....

Klabu ya soka ya Yanga imetinga hatua ya 16 bora ya kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada kupata wa mabao 4-3 kwa njia ya penati

Golikipa Youth Rostand ndiye shujaa wa Yanga kwa siku ya leo baada kupangua penati tatu, na kuiwezesha timu yake kutinga hatua ya 16 bora

Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya, Ihefu inayoshiriki ligi daraja la pili Tanzania chupuchupu walizamishe jahazi la Yanga ndani ya dakika 90, kufuatia kupata bao baada mlinzi wa Yanga Andrew Vicent kujifunga kunako dakika ya 37 ya mchezo

Kuingia kwa bao hilo, kuliwaamsha Yanga na kuanza kusukuma mashambuli ya kasi langoni kwa Ihefu lakini walinzi wake walisimama imara na kuzima mashambulizi ya Yanga

Kipindi cha pili, Yanga waliendelea kusukuma mashambulizi ya mara kwa mara huku wapinzani wao wakionekana kucheza kwa kujihami na kutumia mbinu za kupoteza muda

Yanga ilibidi wasubiri, na ndipo ule usemi wa wahenga wa “paka mzee halimshindi dari” ukatimia, pale mshambuliaji wake Obrey Chirwa kuitafuta penati na kufanikiwa kunako dakika ya 91

Chirwa aliingia kwenye eneo la hatari na kukubali kwenda chini kwa urahisi baada kubanwa na walinza wa Ihefu, ndipo mwamuzi akaamuri penati na Chirwa kufunga penati hiyo kuisawazishia Yanga bao

Ndipo muda wa changamoto za mikwaju ya penati ukawadia, lakini kipa wa Ihefu Andrew Kayuni aliwapagawisha Yanga baada ya kuokoa penati ya kwanza ya Pappy Tshitshimbi

Kelvin Yondan, Hassan Kessy, na Gadier Michael walifunga penati zao kabla ya Chirwa kugongesha mwamba penati ya tano

Raphael Daud alifunga penati ya sita, huku Youth Rostand akidaka penati za Emmanuel Mamba Richard Ngondya na Abubakar Kidungwe, wakati zile za Mando Mkumbwa, Andrey Kayuni na Jonathan Mwaibindi zikitinga nyavuni

Sambaza....