Sambaza....

Baada ya kuibuka na ushindi mbele ya Pamba Fc katika mchezo uliopigwa hapo jana katika Dimba la Benjamin Mkapa ni rasmi sasa nusu fainali ya kombr la FA itawakutanisha vigogo Simba na Yanga.

Simba imefanikiwa kuifunga mabal manne kwa bila Pamba katika mchezo wa robo fainali, mabao ya Simba yalifungwa na Peter Banda, Kibu Denis na Yusuph Mhilu aliefunga mabao mawili.

Kwa ushindi huo Simba anamfwata Yanga nusu fainali ambae alishafuzu kwa kuwatoa Geita Gold kwa mikwaju ya penati baada ya mchezo kumalizika kwa sare ya bao moja moja ndani ya dakika 90.

Tangu kombe hili lirudi Simba amekua na historia nzuri mbele ya Yanga. Simba na Yanga wamekutana mara tatu huku mara zote Simba akiibuka na ushindi. Mara ya mwisho kukutana watani hao katika kombe la FA Simba aliibuka na ushindi wa bao moja bila katika Dimba la Lake Tanganyika Kigoma.

Sambaza....