Sambaza....

Mchezo uliokua unasubiriwa kwa hamu Tanzania na Afrika kwa ujumla hatimae leo April 30 Saa 11 jioni utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa pale Temeke Jijini Dar es salaam.

Ndio Yanga leo atakua mwenyeji wa Simba katika Uwanja wa Mkapa baada ya mchezo wa kwanza kuisha kwa sare ya bila kufungana hapohapo kwa Mkapa. Sipati picha mchezo huu Yanga angekua mwenyeji halafu ngoma inapigwa katika uwanja wao kabisa ambao ungekua Kigamboni, hilo vibe lake sijui ingekuaje haswa katika mchezo muhimu huu wakujihakikishia ubingwa.

Hassan Dilunga (kushoto) akiwania mpira na Djuma Shaban

Kwa nyakati tofauti makocha wa timu zote mbili wametamba na kujinasibu kupata ushindi na alama tatu mbele ya mwenzie.

Kwa upande wa Yanga kocha msaidizi Cedrik Kaze ambae ndio atasimama kwenye benchi ameiita ni mechi “special” na kutanguliza heshima kwa Simba.

Cedrik Kaze ” Hii ni mechi special, unaona hata maandilizi yamekua special hata huu mkutano na Wanahabari umeandaliwa special pia.”

Yanga katika mchezo wa kesho watawakosa Chico Ushindi na Yacouba Sogne pekee wakati Djuma Shaban yeye yuko fiti baada ya kupata shida kidogo katika mchezo dhidi ya Namungo.

Upande wa pili wageni wa mchezo huo Simba kocha Pablo Franco amesema wametoka kucheza mchezo mkubwa lakini bado unaonyesha wao ni bora kiasi gani.

“Sisi tumezoea kucheza mechi kubwa kama hizi, nadhani mliona wenyewe kilichotokea katika robo fainali na ndio maana tunasema sisi ni bora kuliko wao” Pablo Franco.

Wachezaji wa Simba wakiingia uwanjani katika dhidi ya RS Berkane  mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika

Kwa upande wa majeruhi ni Hassan Dilunga pekee ataukosa mchezo huku huku Simba ikipata nguvu na urejeo wa John Bocco katika eneo la ushambuliaji.

Vikosi Vyenyewe!

Yanga!

1. Diara

2. Djuma Shaban

3. Kibwana Shomary

4. Yanick Bangala

5. Mwamnyeto

6. Aucho

7. Farid Mussa

8. Sure Boy

9. Mayelle

10. Feisal.

11. Saidoo

Sub: Mshery, Mustapha, Job, Mauya, Nkane, Makambo, Ngushi.

Fiston Kalala Mayele

Simba!

1. Manula

2. Kapombe

3. Tshabalala

4. Onyango

5. Inonga

6. Mkude

7. Sakho

8. Kanoute

9. Mugalu

10. Chama

11. Morrison

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao pekee walilolipata katika mchezo dhidi ya Orlando Pirates

Sub: Beno, Mwenda, Wawa, Bwalya, Mzamiru, Kagere, Kibu, Bocco.

Ni waz kabisa mbinu za walimu leo ndio zitaamua matokeo lakini pia mifumo ya timu zote mbili ndio itayoamua leo kama mashabiki watapa burudani ama la katika Uwanja wa Mkapa!

Ni  soka la Kihispanyola la Pablo Franco ama ni Profesa Nesradine Nabi kuibuka mbabe!? Muda utaongea!

YouTube player

Sambaza....