Sambaza....

Sina uhakika kama Azam na Yanga wakutanapo ni derby au ni big match ama ni crucial match.
Basi binafsi nitapenda nitumie neno ‘big match’ kwa kuwa crucial kwa Azam ya sasa inaweza isilete maana.


Kwa tamaduni za mwanadamu yeyote na hasa sisi Wabantu famili nyingi zimekuwa na mtoto wa kambo ambaye anatafsri ya moja kwa moja baba alizaa pembeni au nje ya ndoa lakini akamleta yule mtoto kuishi nyumbani akiwa na mke mwingine.

Kumekuwa na simulizi kadha wa kadhaa za unyanyasaji wa mtoto wa aina hii, hasa kukosa upendo na Mama ‘mwenyenyumba’ uwiano wa kazi na majukumu vipaumbele mahitaji na chakula kwa watoto kati ya wa mama mwenyewe na huyu wa kufikia.
Nahodha wa Yanga akipiga shuti mbele ya Idris Mbombo wa Azam Fc.

Japo eneo hili si wote wanaoshi na mama na hata baba wa kambo wamepitia kadhia hizi wapo wachache 25% waliolelewa kwa upendo mkubwa kutoka kwa mama wa aina hiyo kifupi ni zaidi ya bahati.

Nimelazimika kufafanua hili kwa sababu Azam amekua analalamika kanakwamba si mtoto mpendwa wa mamlaka husika za soka ilhali hata akidhulumiwa haki zake hana kwa kukimbilia, hapewi vipaumbele ambavyo wenzake wanapata na wanasema hawana “Direct attachment” na baba wa soka nchini.

Leo wanakwenda kucheza na Yanga Africa katika uwanja wao wa nyumbani Chamanzi,
wanakutana wakiwa katika mazingira mawili tofauti ya “kiperfomce” ndani ya msimu.

Heritier Makambo akieania mpira dhidi ya mlinzi wa Azam Fc Daniel Amoah.

Heritier Makambo akiruka mbele ya mlinzi wa Azam Fc Daniel Amoah
Azam iliyocheza michezo 18 na kushinda 8 sare 4 na kupoteza mara 6 imefunga magoli 22 na kuruhusu magoli 16 utajifunza kitu kwenye balancing ya timu ndiyo maana nilisita kusema ni’ crucial match’.

Yanga imecheza michezo 18 imeshinda 15 imesare 3 ina magoli 31 ya kufunga huku ikiruhusu 4 tu unaweza kupata uwiano wa team ilivyobalance.

Pamoja na Yanga kuwa vizuri kitakwimu haileti maana ya moja kwa moja kwenye kupata matokeo yote yanaweza kusahaulika kwa kuwa huu ni mchezo mwingine kabisa.

Djuma Shaban wa Yanga akimtoka kiungo wa Azam Fc Paul Katema.

Kwanini  kutibua sherehe, sherehe yenyewe ni ipi? Kifupi “mentality” za uongozi wachezaji na mashabiki wa Yanga kwamba mwaka huu ubingwa ni wao huku akitarajia kufanya sherehe kubwa ya kujipongeza.

Huku Simba wao wakiamini nao wanaweza kuwa mabingwa endapo Yanga kupoteza kwa mechi 3-4 ikiwemo hii dhidi ya AzamFc 

Ni kweli watatibua sherehe ya watu
tusubiri tuone!

Sambaza....