Rivers United wameondoka nchini Nigeria kuelekea Dar es Salaam, Tanzania kwa ajili ya mchezo wao wa mkondo wa pili wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Young Africans.
Kikosi cha Pride of Rivers kiliondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Murtala Mohammed, Lagos Alhamisi alasiri. Kikosi cha Stanley Egunma kitalenga kwenda kupindua matokeo baada yakufungwa 2-0 kutoka kwa mkondo wa kwanza.
Mabingwa hao wa NPFL watamenyana na Young Africans katika mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Jumapili. Mshindi katika mchezo huo atamenyana na Pyramids ya Misri au Gallants FC ya Afrika Kusini katika mechi ya nusu fainali.
Awali timu hiyo ilikua katika wakati mgumu wakifedha na kupelekea kuwa na hatihati yakuwahi kuanza safari yakuja nchini na kupelekea kocha wao kukiri huenda wakafika siku moja kabla ya mchezo wenyewe yaani Jumamosi.
Kwa upande wa Yanga wao tayari wapo kambini Avic Kigamboni wakijifua kuelekea mchezo huo wa marudiano wakitafuta rekodi yakucheza nusu fainali ya michuano hiyo.