Sambaza....

Anasema Mzee Lukinja kwa lugha ya upole iliyojawa hekima na busara ndani yake, 
“Asiye shukuru kwa kidogo hata akipewa kikubwa hawezi kushukuru na nyongeza yake asiye mshukuru binadamu mwezake anayemuona kamwe hawezi kumshukuru Mwenyezi Mungu asiye muona.”

Sina hakika kama yupo sahihi lakini Mimi binafsi nashukuru kwa kamati ya tuzo kwa maandalizi mazuri ya tukio zima (event).

Pamoja na tukio kuwa la utoaji tuzo za ujumla, tuzo nyingine huonekana kama mvua ya rasharasha vile ‘main Card ‘ kama ambayo kwenye masumbwi hutumika kutambulisha ukubwa wa pambano lenyewe achilia mbali yale ya utangulizi basi tuzo ya MVP yaani “Most Valuable Player” ama waweza kusema tuzo ya mchezaji bora wa jumla ndiyo kubwa lililoangaziwa.

Bado naendelea kuheshimu mtizamo wa kamati ya tuzo chini ya kaka yangu Msafriri Mgoyi kwenye eneo la MVP kwa vigezo vilivyotumika kumpata mchezaji huyu ni art yake ya uchezaji (sanaa yake).

Yanick Bangala mchezaji bora kwa msimu wa 2021/2022.

Uwezo wa kupokea na kuendeleza mpira kwenye maeneo yote matatu muhimu ya mchezo wa mpira ambayo yanaambatana na ufundi na mbinu ,ili upate Kushambulia na kujihami kwa timu ikiwemo kupita eneo muhimu la idara ya kati (transition).

Kwenye hao wachezaji watatu waliokuwa wametajwa kwenye nafasi hiyo Fiston Mayele ndiyo kwa mtizamo wangu alikuwa anastahili zaidi si kwa uwezo wa kufunga bali ufanisi wa kiuchezaji na hasa anaporudi kuchukua mipira nyuma na kwenda kama si kuhitimisha kwa kufunga basi kupasia wenzake akiwa kawaburuza watu kwenye maeneo haya matatu eneo 1,2 na 3.

Fiston Kalala Mayele.

Kwa hao “nominees” wenzake huwezi pata hivyo vitu vitatu zaidi ya kuwa bora kwenye eneo au waweza kusema ‘wizara zao’ achana na sifa zile zinazoaminika kwamba mchezaji bora anapaswa kuwa na B3.

Yawezekana wote wakawa na B3 lakini tunakuja kwenye kuzitumia naona Mayele alistahili.

Pia kikosi bora cha msimu acha miye nikibariki kwamba kuteuzi wake umekuwa mzuri na yawezekana umezingatia sana hofu ni kwa kijana Abdul Sopu kuwemo kama ukiangalia play style yake na dhidi ya wengie walioachwa kuna ukakasi kidogo ,pia tunapozungumzia tuzo ya NBC ni lazima tujikite kwenye Performance ya ligi hiyo tu ,tusichanganye mafaili na Azam Sports federation Cup ambapo kule aliwaka kweli!

Eneo jingine lenye ukakasi kwangu ni tuzo ya mchezaji wa Championship (zamani ligi daraja la kwanza) na ile ya first ligi (zamani daraja la pili).

Ukiangalia Abdul Sopu anatajwa kuwa mchezaji bora wa ASFC akiwa pia amemaliza na goli 9 ikiwemo hati trick dhidi ya Yanga binafsi naamini uwezo wa kufunga au kuwa mfungaji bora ndiyo kumepelekea pia awe mchezaji bora.

Kama ilivyo kwa Edward Songo yule wa JKT Tanzania aliyemaliza na goli 14 akashinda tuzo ya mchezaji bora toka championship.

Tuliporudi kwenye mchezaji bora wa first league akatawa golikipa wa Copco united ya Mwanza Mohammed Azizi Hussein akimpita mfungaji bora wa ligi hiyo Seleman Kibuta aliyemaliza msimu akiwa na goli 18.

Ukiangalia unaona kuna muda wanaingia kwenye sifa ya mchezaji bora kuangaliwa kutokana na magoli aliyoyafunga kuna muda wanachoropoka kuavoid hoja ya kukosekana kwa George Mpole kwenye shortlist ya MVP

Kuna jambo jingine linaleta ukakasi kwenye mchezaji bora wa Championship huyu golikipa ambaye michuano wakati imeisha kulikuwa na tuzo pia mshindi akawa golikipa wa Mbuni Yasin Mgaza lakin siku ya mwisho huku kwenye ngazi ya mwisho kaibuka ambaye alipitwa kwenye ngazi za awali.

Haina shaka tuendelee kujifunza nakujipanga tukiboresha dosari ndogondogo wakati mwingine tutakuwa bora zaidi.

Sambaza....