Sambaza....

 

Mwinyi Zahera alipata nafasi ya kuitazama timu yake ya zamani ya Yanga kwenye mechi yao ambayo waliyocheza dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Taifa na mechi ikaisha kwa sare ya 1-1.

Katika mechi hiyo goli la Yanga lilifungwa na Bernard Morrison mchezaji ambaye amesajiliwa kipindi cha kocha wa sasa wa Yanga , Luc Eymael.

Baada ya mchezo huo Mwinyi Zahera aliulizwa namna alivyomuona Bernard Morrison katika mchezo huo na jinsi anavyoisaidia Yanga .

Mwinyi Zahera alidai kuwa alitaka aina ya wachezaji kama Bernard Morrison Lakini hakupewa hela ya kusajili wachezaji ambao aliwataka kwenye mfumo wake .

“Kwenye mikutano ya waandishi wa habari niliwaambia kuwa nahitaji wachezaji wa pembeni wenye kasi , wanaopiga Chenga na kupiga krosi kama Bernard Morrison”- alisema kocha huyo wa zamani wa Yanga.

Kocha huyo alidai kuwa falsafa yake ilikuwa inahitaji mchezaji kama Bernard Morrison na alikuwa analisema mara kwa mara kipindi alipokuwa kocha mkuu wa Yanga.

“Kila siku nilikuwa nawaambia kuwa falsafa yangu inahitaji mchezaji kama Bernard Morrison , Lakini sikuwahi kupata nafasi ya kusajili kwa sababu timu haikuwa na pesa”- alimalizia kocha huyo wa zamani wa Yanga

Sambaza....