Timu ya Bonbon Ndjema fc wakiwa tayari na tiketi ya ushiriki wa Mashindano ya Kimataifa ambao wanasubiri kupangiwa mpinzani kama ambavyo Simba na Namungo kwa huku kwetu wanavyosubiri.
Wakizungumza na mtandao wa Kandanda.co.tz muda mchache kabla ya kusafiri kuelekea kisiwa cha Anjuwani katika mchezo wao wa kombe la mabingwa wa visiwa vya Comoro wamejinasibu kujiandaa vyema kwa Mashindano hayo pamoja na Michuano ya Caf itakapoanza.
Akizungumza na tovuti hii Senetor wa timu hiyo Mr Sovek amejigamba kufanya vyema licha ya mabadiliko kadhaa kwenye benchi la ufundi ambapo walimtimua Kocha mkuu na kwa sasa timu ipo chini ya Kocha msaidizi Sumeti ambaye anaiongoza vyema tangu alivyochukua mikoba hiyo.
Mr. Sovek ” Tulimfukuza kocha mkuu lakini haitufanyi kushindwa kuendelea kufanya mambo mazuri Ligi ya Mabingwa. Tumejiandaa vyema tupo tayari kupambana katika Ligi hiyo ambapo huko Tanzania naskia Simba watashiriki pia.”
Lakini pia Kocha Sumeti anajivunia uwepo ya mshambuliaji wake bora Basleri ambaye anawastani wa kufunga goli moja kwa mechi mbili kitu ambacho ni kizuri sana kwa takwimu za mshambuliaji na kwa timu pia.
“Kocha mkuu aliondoka kwasasa bado naendelea na timu, tupu vizuri tuna wachezaju wazuri. Najivuni mshambuliaji wangu Basler anatusaidia sana kwenye ufungaji wa mabao. Ukitazama hata wastani wake katika ufungaji kwenye Ligi unaona kabisa takwimu zinambeba.” Sumeti.
Mwalim huyo pia hakusita kumpongeza Mr Sovek ambae ni mwenyekiti wa timu hiyo Salim Timturibo ambaye amekuwa akijitoa vilivyo katika kutaka mafanikio ya timu yake.
Timu hii imewahi kumsajili mchezaji toka Tanzania Boniface Nyagawa toka Mbeya kwanza ambaye baadaye alitimukia kwa wapinzani wao Ngaya Fc ambayo miaka mitatu iliyopita waliwahi kuja nchini kucheza na Yanga katika mashindano ya ligi ya mabingwa wa Africa chini ya CAF.