Hatimaye Kariakoo Derby imeisha , imeisha katika mazingira ambayo yalikuwa ni mazingira sahihi kwa kila upande , sare ilikuwa sahihi kwa timu mbili , lakini pamoja na upatikanaji wa ile Sare , kuna baadhi ya Simba wachezaji wa Simba ambao walikuwa wanacheza maeneo muhimu hawakuwa kwenye kiwango bora.
MEDDIE KAGERE
Sawa alisababisha na kufunga penalti katika mchezo wa jana , lakini hakuwa Meddie Kagere ambaye tulimzoea kumuona kila Siku . Meddie Kagere ambaye huwafanya mabeki wa timu pinzani wawe na muda mwingi wa kumlinda tu. Lakini jana mabeki wa kati Wa Yanga muda mwingi walikuwa wanatumia kuanzisha mashambulizi na muda mchache kumlinda , Meddie Kagere aliwafanya mabeki wa Yanga kuwa sehemu ya uanzilishi wa mashambulizi.
FRANCIS KAHATA
Alitoa pasi iliyosababisha Penalti jana , lakini hakuwa na kiwango bora kama tulivyomzoea Siku zote. Alimfanya Juma Abdul kutokuwa na uwoga wa kwenda kuisaidia timu kushambulia . Juma Abdul alikuwa na nafasi kubwa ya kushiliki kushambulia kuliko kumlinda yeye hivo na kuwafanya Yanga waongeze watu wakati wa kushambulia.
SHOMARI KAPOMBE
Jana hakuwa Shomari yule , pamoja na kwamba aliahikiriki kutengeneza nafasi ya goli la pili , lakini hakuwa kwenye kiwango chake bora , eneo lake kuna wakati lilikuwa na uwazi sana hata goli la pili la Yanga limetokea eneo lake , mpigaji wa krosi alikuwa huru . Tumemzoea Shomari Kapombe kama mchezaji anayepanda kushambulia na kushuka kukaba kwa pumzi ile ile lakini jana haikuwa hivo.
CHAMA
Huyu sijui kipi kimempata , hayupo vile kama alivyokuwa awali , jana hakuwa anachezesha timu vizuri kama ilivyozoeleka kutoka kwake . Pia tumemzoea Chama ni mchezaji ambaye anafanya HIGH PRESSING , Lakini kwenye mechi ya Jana hakuwa anafanya HIGH PRESSING, kitu ambacho kilikuwa kinawapa nafasi mabeki wa kati wa Yanga kushiriki katika uanzilishi wa mashambulizi.