Emmanuel Amunike siku ya Jumamosi alikuwa kwenye mtihani wake wa kwanza akiwa kama kocha wa timu ya taifa ya Tanzania “taifa stars”.
Mechi ambayo ilikuwa ngumu kwa sababu Uganda walikuwa na rekodi nzuri dhidi yetu na pia Uganda walikuwa wanaongoza kundi.
Na kibaya zaidi Uganda alikuwa nyumbani, uwanja ambao umekuwa mgumu kwa kila timu ambayo ilikuwa inakanyaga katika ardhi ya Uganda.
Kabla ya kwenda Uganda, kuna wachezaji wa Simba waliondolewa kwenye orodha ya wachezaji wa timu ya taifa baada ya kuchelewa kambi.
Wachezaji hao wengi walikuwa wa klabu ya Simba ambao ni John Bocco, Shiza kichuya, Jonas Mkude, Erasto Nyoni,na Shomari Kapombe.
Wengi walikuwa na hofu kwa sababu wachezaji hawa walionekana muhimu sana.
Je kuna baadhi ya wachezaji ambao walistahili kuanza siku hiyo?.
Kwa jinsi ambavyo niliangalia mechi ya hii kuna wachezaji wawili (2) ambao walistahili kuanza katika mechi hii.
Wachezaji hao ni Erasto Nyoni na Jonas Mkude.
Kwanini hawa wachezaji wawili?
Emmanuel Amunike alianza na mfumo wa mabeki watatu(3) yani mfumo wa 3-4-3.
Kikawaida katika mfumo huu ni muhimu (siyo lazima) ila ni muhimu kuwa na mabeki ambao wanaweza kumiliki mpira na kupiga pasi.
Mabeki ambao walianza Jana hawakuwa na uwezo wa kumiliki mpira na kupiga pasi kwa kiasi kikubwa.
Hivo Erasto Nyoni alikuwa muhimu sana kuanza katika mechi ya Jana kwa sababu anasifa za kumiliki mpira na kupiga Pasi.
Kwanini Jonas Mkude?
Jana Emmanuel Amunike alikuwa na nia ya kujilinda kwa muda mwingi na kushambulia kwa tahadhali ndiyo maana alianzisha viungo wawili wenye asili ya kuzuia ( Mudathir Yahaya na Frank Domayo).
Jonas Mkude ni kiungo ambaye ana asili ya kuzuia pia. Ila anasifa moja ya ziada ambayo viungo walioanza waliikosa nayo ni ya Ku “command” timu.
Yupi alistahili kuwepo kipindi cha pili ?
Kwa dakika 15 za mwishoni Taifa Stars ilianza kufunguka kwenda mbele. Ndiyo dakika ambazo Taifa Stars ilihitaji goli. Lakini ilikosa vitu viwili.
Cha kwanza kiungo anayetokea katikati ya uwanja ambaye angeweza kutengeneza nafasi na kufunga akitokea katika ya uwanja , hivo dakika 15 za mwishoni Shiza Ramadhani Kichuya zilimhusu.
Kitu cha pili, Taifa Stars ilihitaji “poacher” mchezaji ambaye angesimama eneo la kati bila kuhama ili akutane na mpira ambayo ilikuwa inafika eneo la mbele. Hapo ndipo John Bocco alitakiwa kuwepo kwa dakika 15 za mwisho.
Kwa game approach ya Emmanuel Amunike, ilikuwa ni ngumu kwa John Bocco na Shizà Kichuya kwa sababu Emmanuel Amunike alikuwa na mpango wa kujizuia kwa asilimia kubwa, ndiyo maana alianza na wachezaji wengi wenye asili ya kujilinda.