Maelezo hata ya kina kwa ufupi yameandaliwa na Yossima Jr, hatujarekebisha kitu.
-Aliyozungumza CEO wa klabu ya Simba kwenye mkutano na waandishi wa habari leo ni Mchakato wa mabadiliko, Ujenzi wa viwanja vya Simba Bunju, Jezi mpya za klabu ya Simba msimu ujao, Mambo ya Usajili, Wiki ya Simba kuelekea tamasha la Simba day August 08, Wimbo maalumu wa klabu ya Simba, Vifaa mbalimbali vya Simba na Nafasi yake ya UCEO ndani ya klabu ya Simba
-Kuhusu mchakato wa mabadiliko Magori amesema kuwa Bodi ya wakurugenzi imeunda timu ya watu wanne kukamilisha baadhi ya vitu vilivyobaki kwenye mchakato ndani ya mwezi mmoja jambo hilo liwe kimekamilika.
-Ujenzi wa viwanja vya Simba Bunju (Bunju Project) Ceo amesema kuwa Bodi imemteua aliyekua meneja wa klabu ya Simba, Robert Richard kuwa msimamizi wa project hiyo ambayo inatarajia kukamilika ndani ya mwezi mmoja ikiwa kuweka zulia kwa uwanja wa nyasi bandia na kutengeneza uwanja wa nyasi za kawaida pamoja na ujenzi wa choo na vyumba vya kubadilishia nguo.
-Jezi Mpya kampuni ya Uhlsport ndio imeshinda tenda ndani ya siku 3 watasaini mkataba mpya na kampuni hiyo kuhusu kutoa na kusambaza vifaa vya Simba. Pia Simba imesema itatangaza dau na muda wa mkataba huo na kampuni hiyo kuhusu mkataba na watazindua jezi 3 za msimu ujao.
-Kuhusu Usajili CEO, Magori amesema wachezaji wote ambao wanapaswa kuongezewa mikataba ndani ya Simba ulishakamilika sasa ni jambo la kutangaza tu na pia wachezaji wa ndani ambao kocha aliwataka wasajiliwe usajili wao ulishakamilika kinachosubiliwa ni kutangazwa. kuhusu wachezaji wa nje CEO Magori amesema kwa sasa ndio wanasajili wachezaji wa nje na kuanzia wiki ijayo wataanza kuwatangaza.
-Kuelekea tamasha la Simba day, Magori amesema kuwa tayari walishakubaliana na klabu moja kubwa kutoka Afrika Magharibi ambayo itakuja kucheza na Simba siku ya Simba Day August 08. Kuhusu wimbo maalumu wa Simba, Magori amesema Afisa Habari wa klabu hiyo Haji Manara amepewa jukumu la Kuratibu waimbaji wote wale ambao ni wapenzi wa Simba watatunga wimbo maalumu wa Simba ambao utazinduliwa siku chache kabla ya wiki ya Simba.
-Vifaa mbalimbali vya Simba, CEO Magori amesema bodi imebariki maombi mbalimbali ya wanachama wa klabu hiyo kuhusu kutengeneza vifaa mbalimbali vya Simba vikiwemo nguo za wanawake kama kanga, Madela na nk. Magoli amesema Kampuni itakuwa inatengeneza jezi itapewa kazi hiyo ili kuanzia msimu ujao iuze vifaa mbalimbali.
-Nafasi yake ya CEO ndani ya klabu ya Simba, Magori amekili ni kweli muda wale wa uongozi ndani ya klabu ya Simba umeisha mwezi wa 5 mwishoni ila kwenye kikao cha bodi cha jana wamekubaliana kumuongezea muda wa miezi miwili huku mchakato wa kutafuta CEO mpya na wakurungezi wengine wanne ukifanyika baada ya miezi miwili mchakato huo utakuwa umekamilika ndani ya siku 3-10 Simba watatangaza nafasi mbalimbali za kazi wenye vigezo waweze kuomba.
@Yossima Jr.