Sambaza....

KATIKA siku ambayo Geilson Santos Santana ‘Jaja’ alifunga mabao mawili maridadi sana dhidi ya Azam FC na kuisaidia timu yake ya Yanga SC kutwaa taji la Ngao ya Jamii, Agosti, 2014 wengi walitaraji kuona muendelezo wa magoli ya kuvutia kutoka kwa ‘namba 9’ wa kwanza kutoka Brazil katika soka la Tanzania.

Mashabiki wa Yanga walisikika wakiimba na kulitamka jina la Mbrazil huyo-Jaja huku wakimponda aliyekuwa mchezaji wao Emmanuel Okwi aliyekuwa amerejea Simba SC akitokea Yanga katika usajili wa katikati yam waka 2014.

Wilker Henrique da Silva

Akisimama kama mshambulizi huru katika mfumo wa 4-5-1, Jaja alifunga goli kali akiwa katikati ya walinzi wa Azam FC akiunganisha kiustadi krosi pasi ya Saimon Msuva kutoka winga ya kulia. Baadae akafunga kwa stahili ya mshambulizi kwa pasi safi ya kupenyeza kutoka kwa Mrisho Ngassa.

Kuanzia hapo, wengi waliweka matarajio makubwa kwa mchezaji huyo kuliko Mbrazil mwenzake Andrey Coutinho.Jaja alikuwa Tanzania akiwa tayari amepevuka kiumri kuliko Coutinho lakini kiwango chake hakikuwahi kuwavutia wengi.

Baadae akaanza kuzomewa hadi na mashabiki wa klabu yake mwenyewe jambo lililomfanya kupunguza hali ya kujiamini, akapoteza furaha na kufikia Novemba, 2014 aliomba kwa klabu kusitisha mkataba. Licha ya kufunga magoli mazuri vs Azam FC, Jaja alifunga mara tat utu katika Zaidi ya michezo tisa uiliyofuata huku uwezo wake wa kumiliki mpira ukuonekana tatizo hasa katika viwanja wa mikoani.

WABRAZIL WA SIMBA…..

Beki wa kati mwenye umri wa miaka 30, Tairone Santos da Silva amesaini mkataba wa miaka miwili klabuni Simba, haitoshi, mshambulizi, Wilker Henrique da Silva mwenye miaka 23 na kiungo-mlinzi, Gerson Fraga Viera mwenye miaka 26 wote hawa inasemekana ni mapendekezo ya kocha mkuu wa klabu hiyo, Mbelgiji, Patrick Aussems.

Gerson Fraga Vieira

Kuondoka kwa kiungo kama James Kotei raia wa Ghana ambaye sit u alishinda tuzo ya mchezaji bora wa nafasi ya kiungo kwa klabu yake msimu uliopita bali aliyekuwa akionyesha kujituma uwanjani, unataraji kuona mbadala wake anapaswa kuwa juu kwa namna gani.

Wabrazil ni wataalamu wa soka- hilo liko wazi lakini naamini Simba ilipaswa kujifunza kwanza kwa yale yaliyowakutana Yanga hasa kwa Jaja. Kama wachezaji hao watafikia angalau asilimia 50 tu ya viwango vyao vya kawaida bila shaka utakuwa usajili mzuri kwa timu lakini kitendo chochote cha kushindwa kufikia ubora ulioachwa na Kotei sitashangaa mashabiki wa Simba wenyewe kuanza kuwazomea wachezaji wao hao kutoka Brazil.

Simba ilifikiria kuwasaini wachezaji kama Watler Bwalya, Jakaka Tuyisenge, Jean Mundele Makussu lakini wamewakosa wote hao labda ndio maana wamekimbilia Brazil kwa kuamini huko kuna vipaji vya kutosha. Nini watafanya? Ni jambo la kusubiri na kuona. Waje kuwa kina Jaja wengine.

Sambaza....