Mshambuliaji Wabrazil anaekipiga katika klabu ya Real Madrid Vinicious Junior amesema anacheza katika Ligi ambayo rangi nyeusi ni tatizo kwao, akiamini watu wa Hispania ni wabaguzi sugu wa rangi.
Vinni katika mchezo kati ya Real Madrid alitolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo baada yakuanza kuzozana kufuatia viashiria vya ubaguzi wa rangi katika mchezo huo vilivyofanya na mashabiki wa Valencia.
Michuano ambayo hapo awali ilikuwa ya Ronaldinho, Ronaldo, Cristiano na Messi leo ni ya wabaguzi wa rangi. Haikuwa mara ya kwanza, wala ya pili, wala ya tatu. Ubaguzi wa rangi ni jambo la kawaida kwenye La Liga. Wasimamizi wa mashindano hayo wanafikiri ni jambo la kawaida, Shirikisho na wapinzani pia wanaendekeza suala hili,” aliandika katika ukurasa wake wa instagram na kuongeza
“Taifa zuri, ambalo lilinikaribisha na ninalipenda, lakini limekubali kuonekana kama nchi ya kibaguzi duniani. Samahani kwa Wahispania ambao hawakubalian na mimi, lakini leo hii huko Brazil, Uhispania inajulikana kama nchi ya wabaguzi.
“Cha kusikitisha kwa bahati mbaya,ni kitu kinachotokea kila wiki, sina mtetezi. Ninakubali. Lakini nina nguvu na nitaenda hadi mwisho kupaza sauti dhidi ya wabaguzi. Hata kama ni mbali na hapa.”
Vinicius si mara yake yakwanza kukutana na vitendo hivyo vyakibaguzi imekua ni mara kwa mara akikutana na mashabiki wa aina hiyo katika michezo ya Laliga. Nae kocha wake Carlo Ancheloti amesema “Tulichokiona leo hakikubaliki uwanja mzima ukiimba kashfa za kibaguzi. Sitaki kuzungumzia soka leo, hakuna maana kuzungumzia soka leo, nilimwambia mwamuzi alipaswa kusimamisha mechi.”
“La Liga ina tatizo. Kwangu mimi Vinicius ndiye mchezaji muhimu zaidi duniani. Vipindi hivi vya ubaguzi wa rangi lazima visimamishe mechi.,” alimalizia Anchelotti