Sambaza....

Mjadala wa Kitaifa kwasasa ni idadi ya wachezaji wa kigeni wanaotakiwa kusajiliwa na timu moja baada ya kuonekana idadi ya wachezaji 10 ni kubwa kwa nchi yetu na inaathiri timu ya Taifa na afya ya soka letu kwa ujumla.

Ili kuwa na timu ya Taifa imara ni lazima uwe na Ligi imara pia au uwe na idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje watakaounda timu ya Taifa haswa kwa nchi zetu za Kiafrika.

Ditram Nchimbi akimkimbiza mlinzi wa Simba Tairone Santos

Katika timu yetu ya Taifa “Taifa Stars kwa miaka mingi timu za Simba na Yanga zimekua zikitoa idadi kubwa ya wachezaji kuunda kikosi cha Stars. Lakini pia timu hizi mbili ndio zinaongoza kua na idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni katika vikosi vyao, hivyo hata huu mjadala wa wachezaji wa kigenu kwa kiasi kikubwa unawagusa wao moja kwa moja.

Mara nyingi wamekua wakisajili wachezaji wengi wa kigeni wakiamani ndio watakaowapa mafanikio katika michuano ya Kimataifa. Wakiamini muunganiko wa wachezaji wazawa na wachezaji wa nje wenye uzoefu ndio utakaounda kikosi imara kupambana na vilabu vikubwa kama Al-Ahly, TP Mazembe, Orlando Pirates na vingine.

John Bocco akiwa katika harakati za kumtoka mlinzi wa TP Mazembe.

Tumekuwekea vikosi vya timu hizi mbili Simba na Yanga wakiwa na wachezaji wazawa watupu bila wachezaji wa kigeni!!

Kikosi cha Simba

  1. Aishi Manula
  2. Shomary Kapombe
  3. Mohamed Hussein
  4. Kennedy Juma
  5. Erasto Nyoni
  6. Jonas Mkude
  7. Miraj Athuman
  8. Mzamiru Yassin
  9. John Bocco
  10. Said Ndemla
  11. Hassan Dilunga

Hao ndio kikosi cha kwanza halafu nje utakua na wachezaji wa akiba kama:

➡️ Benno Kakolanya, Haruna Shamte, Yusuph Mlipili, Shiza Kichuya, Rashid Juma na Gadiel Michael. 

Mzamiru Yassin.

Kwa upande wa Yanga kikosi kitakua hivi!

  1. Menata Mchata
  2. Juma Abdul
  3. Japhary Mohamed
  4. Said Makapu
  5. Kelvin Yondani
  6. Abdulaziz Makame
  7. Deus Kaseke
  8. Feisal Salum
  9. Ditram Nchimbi
  10. Balama Mapinduzi
  11. Mrisho Ngassa

Katika benchi watakua wanasubiri kina:

➡️ Ramadhani  Kabwili, Paul Godfrey, Adeyum Saleh, Andrew Vicent, Juma Mahadhi, Raphael Daud na Mo Banka.

Andrew Vicent Chikupe “Dante”

Kwa vikosi hivyo unadhani vina nguvu ya kupambana na kushinda Ligi ya ndani pamoja na kikombe cha FA?

Je vikosi hivi vitaweza kutoa ushindani katika michuano ya Kimataifa kwa maana ya Klabu Bingwa Africa na Kombe la Shirikisho? Watatoa ushindani kwa vilabu kama AS Vita, Mamelody Sundown, Al Hilal na Horoya fc?

Tupe maoni yako hapa unadhani ni idadi ipi itafaa kwa wachezaji wa kigeni katika timu zetu!

Sambaza....