Sambaza....

 

Moja ya kitu ambacho kwa sasa Yanga kinawauma sana ni kuiona Simba ikiwa na uwanja wake wa mazoezi. Hiki kinawauma sana , ikizingatia wao hawana kiwanja na pia Simba ni wapinzani wao wakubwa sana.

Kitu kibaya ambacho Yanga watakifanya kwa sasa ni wao kuendelea kukaaa chini huku wakiumia kwa Simba kuwa na kiwanja chake , siyo vibaya kwao wao kuendelea kuimua lakini maumivu yawe maumivu yenye faida.

Yanga wayatumie maumivu hayo kwa ajili ya kufikiria namna gani na wao wakafikia kwenye mafanikio hayo ambayo Simba wameyafikia. Wanatakiwa kufikiria namna gani ya wao kuja na kiwanja tena bora zaidi ya kiwanja cha Simba.

Yanga tayari wana kiwanja eneo la Kigamboni , kiwanja walichopewa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , eneo ambalo wanampango wa kujenga kiwanja pamoja na academy ya wachezaji wadogo kwa ajili ya kuibua na kukuza vipaji.

Yanga wanatakiwa kukaa chini na kuja na kitu sahihi cha kuwawezesha wao kufanya vizuri. Cha kwanza Yanga wanatakiwa wakubali kuingia kwenye mabadiliko ya uendeshaji wa timu. Timu iendeshwe kibiashara.

Faida moja kubwa ya timu kuendeshwa kibiashara ni kujenga uaminifu kwenye macho ya watu na kuleta urahisi wa kukopesheka pamoja na wadhamini kuja kuwekeza kwenye timu.

Arsenal Holding PLC ndiyo kampuni inayoimiliki Arsenal , Arsenal Holding PLC ndiyo iliyoenda kwenye milango ya mabenki mbalimbali kwa ajili ya kuomba mkopo wa kujenga uwanja mpya ambao kwa sasa unaitwa Emirates.

Haikwenda Arsenal , ilienda Arsenal Holding plc kama kampuni la kibiashara la mpira wa miguu , huu ndiyo mwanzo ambao Yanga wanatakiwa waaanze nao. Wajitoe kwenye uendeshaji huu walionao , wajenge taasisi au kampuni ndani ya Yanga litakalo aminiwa.

Baada ya hapo ni rahisi kwao kwenda kuomba mkopo kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wao. Wakiomba mkopo wakajenga uwanja , wanaweza wakaingia ubia na kampuni yoyote kwa ajili ya kuita jina la uwanja kwa kutumia jina la kampuni hiyo kwa makubaliano ya kibiashara.

Arsenal waliingia na Fly Emirates , kuita uwanja wao Emirates Stadium , fedha zilizopatikana zilisaidia kulipa deni la uwanja. Mkataba wao unaisha 2028 na Arsenal wameshalipa deni lote la uwanja.

Yanga wanaweza kutumia njia hiyo. Au wanaweza kuwafuata shirika la nyumba la Taifa , au NSSF au taasisi yoyote kama Rwanda Air wao kama wao wakajenga uwanja wa Yanga na wakakubaliana uwanja ule uitwe jina Lao . Mfano NSSF Stadium , NHC Stadium , Rwanda Air Stadium.

Hapa watakuwa wamewazidi Simba ambao wametumia jina la mmoja wa wawamiliki wa Simba , hawajanufaika kwa kiasi kikubwa kibiashara , Yanga wanatakiwa wafikirie namna gani watakavyonufaika kibiashara.

Sambaza....