Sambaza....

 

Kuna hadithi nyingi sana ambazo ziko wazi kwenye dunia hii , hadithi ambazo zimejumuisha mashujaa wetu , hadithi ambazo zimeandikwa kwenye vitabu mbalimbali na pengine hadithi hizi zimewekewa alama ya ukumbusho ili kuwakumbuka na kuwapa heshima mashujaa wetu.

Kumbukumbu zangu zinanikumbusha mzee mmoja anayeitwa Santiago Bernabeu, mzee ambaye enzi za ujana wake aliwahi kuwa mshambuliaji wa Realmadrid , lakini inawezekana hakuweza kufanya makubwa ndani ya klabu ya Realmadrid kama mchezaji.

Lakini aliweza kufanya vizuri sana akiwa katika uongozi kama raisi wa Realmadrid , huyu ndiye mwanzilishi wa Galactico , alianzisha Sara ya Galactico ( sera ya kukusanya wachezaji nyota wakubwa wenye vipaji vikubwa kuja kucheza Realmadrid).

Awamu ya kwanza ya Galactico ilianzia kwake ya Galactico ilianza 1950 – 1960 , ndiyo awamu ambayo tuliishuhudia Realmadrid ikisajili nyota kama Alfredo Di Stéfano, Ferenc Puskás, Raymond Kopa, José Santamaría na Francisco Gento. Nyota ambao walisababisha Realmadrid kuchukua mataji 12 ya La Liga na mataji 6 ya European Club.

Heshima ya Realmadrid ilikuwa kubwa , Realmadrid wakaamua kumpa heshima Santiago Bernabeu heshima kwa jina lake kutumika kwenye uwanja mkuu wa Realmadrid kwa sababu ya kuleta wazo lililoleta mapinduzi ndani ya Realmadrid.

Hassan Dalali alikuwa na wazo kubwa sana awali la Simba kuwa na kiwanja chake , hiki kilimuumiza sana kichwa . Akaamua kutafuta namna ya kufanya Simba ipate pesa ya kiwanja . Alizunguka sana lakini hakufanikiwa.

Wakati akiwa mwenyekiti wa klabu ya Simba alikuja na wazo la Simba Day mwaka 2009 , huyu ndiye mwanzilishi wa Simba Day. Lengo la Simba Day ni kupata fedha za kununua kiwanja ambacho kitatumika kama kiwanja cha Simba.

Mzee wa watu alifanikiwa , alipata milioni 50 ambazo zilienda kununulia kiwanja kule Bunju , Simba ikawa na sehemu ya kuanzia , Ismael Aden Rage alienda milioni 30 kwa Jakaya Kikwete kipindi hicho akiwa Rais kwa ajili ya kupata hatimiliki ya kiwanja.

Rais Jakaya Kikwete aliwapa milioni 30, na Simba wakaitumia kupata hatimiliki ya kiwanja , kiwanja ambacho Leo hii Simba wanakitumia kufanya mazoezi . Kiwanja ambacho mwanzilishi wake ni shujaa Hassan Dalali.

Wazo lake la ushujaa lilistahili kuenziwa kwa uwanja huo kupewa jina lake , wazo lake la Simba Day ndiyo wazo ambalo limetengeneza Simba Day kuwa tamasha kubwa sana kwa sasa hapa nchini. Kwa mawazo haya makubwa yalifaa uwanja wa Simba uitwe jina lake na siyo Mo Arena.

Sambaza....