Kwenye vipengele tofauti hadi shemeji yangu (mke wa Fiston Mayele) mwakilishi wake alivyokuwa anakwenda na kurudi kwenye jukwaa la tuzo kama angenyoosha safari angefika Kibaha hivi (utani kidogo).
Kwa asilimia kubwa Duniani tuzo za jamii hizi huwa nivigumu sana kupokelewa moja kwa moja na wadau kutokana na mitizamo na matarajio ya wengi kwenda ndivyo sivyo.
Binafsi niseme mchakato umekuwa mzuri na umeniridhisha kwa zaidi ya 90+% kama kuna mapungufu ni madogo yana nafasi ya kuangaliwa kwa wakati ujao.
Kitu kipya nilichokiona ni attention ya watu kwenye mshindi wa tuzo ya mfungaji bora badala ya MVP (mchezaji bora wa Ligi) kama ambayo imezoeleka kote.
Nikawaza kwa haraka hii inatokana na “Nominees” kutoka kwenye vilabu vikubwa vyenye ushawishi au la?
Nikajiuliza mfano hali hii imetokea mchezaji mmoja toka kwenye timu zetu za Kariakoo na mwingine labda Mbeya city hii gumzo lingekuwa kubwa kiasi hichi?
Mwisho wa siku niwapongeze kamati kwa uratibu mzuri wa shughuli nzima walioshinda wale ambao kura hazijatosha wana nafasi ya kufanya vizuri wakati mwingine waendelee kukaza.
Katika usiku ule Fiston Mayele alibeba tuzo tatu, Mayele ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu, mfungaji bora wa ligi na goli bora la msimu.