Sambaza....

Kocha wa timu ya soka ya Mwadui ya Shinyanga Ali Bizimungu ametaja mipango yao ya msimu baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye  mchezo wa ligi kuu uliofanyika Jumapili hii.

Bizimungu amesema matokeo hayo ni kama chachu ya kufikia malengo yake ambayo ni kushika nafasa saba za juu katika msimamo wa ligi hiyo ambayo inashirikisha jumla ya timu 20.

“Hatutaki kufanya kitu cha kubahatisha, afadhali tubaki katika timu afadhali saba bora, na ukiangalia kuna wachezaji wetu wamerudi kutoka kwenye majeruhi na tumeongeza wachezaji wawili, ni kama kusema tu sasa mashabiki watoke majumbani kwao waje kusherehekea na sisi ushindi kila mchezo,”

Amesema baada ya matokeo hayo sasa anajiandaa na mchezo ujao dhidi ya Singida United ambao anaamini vijana wake watajituma na kutafuta ushindi ili kuendelea kujiweka katika msimamo wa ligi.

“Kwetu kila mechi ni kama fainali, tunataka kila mchezo kuwa bora, kwa kucheza vizuri na kwa kumiliki mpira, hivyo kila mechi tunajiandaa kupata ushindi, Singida ni timu nzuri ilitufungwa kwao bao moja, hatukufurahi, hapa nyumbani tutafuta namna yoyote tunajua wanavyocheza tupate ushindi,” amesema.

Ushindi dhidi ya Kagera Sugar wa mabao 4-0 unawafanya Mwadui kufikisha alama 24 baada ya kucheza michezo 20 na kuchumpa hadi nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Sambaza....