Katika usajili duniani kote huwa ni kama kitendo cha kucheza kamari kwa maana unaweza ukamsajili mchezaji mzuri lakini akija katika timu yako anakua mchezaji wa kawaida au wa hovyo kabisa na kushindwa kukupa kile ulichotarajia.
Miongoni mwa Ligi zinazopendwa na kifwatiliwa na watu wengi wapenda soka nchini ni pamoja na VPL, EPL, Seria A na Laliga ambapo watu wamegawanyika makundi kwa kusapoti timu maarufu kama Simba na Yanga, Real Madrid na Barcelona, Juventus, Inter Milan na AC Milan Manchester United, J Liverpool, Chelsea na Aston Villa.
Katika ligi hizo timu zimekua zikifanya sajili ili kuboresha vikosi vyao huku wengine wakilamba dume lakini wengine wakipoteza. Miongoni mwa timu zilizofanya usajili katika dirisha dogo katika pendwa EPL, VPL na Seria A
Makala hii inakuletea baadhi ya sajili ambazo zimeonekana kulipa na wachezaji kuingia moja kwa moja katika vikosi vya kwanza na kuleta faidi katika timu ambapo kama wangesajiliwa mapema huenda kwa mchango wao wangekua timu zao zingekua mbali zaidi.
Mbwana Samatta- Aston Villa.
Amesajiliwa na Villa akitokea Genk kwa ada ya pauni milioni 8.5 akitokea KRC Genk kwa mkataba wa miaka minne na nusu. Amefanikiwa kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza wa Epl na pia katika fainali ya Carabao Cup. Mpaka sasa Villa ni ya19 katika msimamo, kwa ujio wa Samatta katika safu ya ushambuliaji kumeongeza kitu na kama angesajiliwa mapema Villa huenda isingekua katika eneo la kushuka daraja.
Bruno Fernandes- Manchester United.
Usajili wake ukichelewa na kua na utata mwingi huku ikionekana Man U hawataki kutoa kiasi kikubwa cha pesa walichokua wanataka Sporting Lisbon ili kumuachia nyots huyo. Lakini mpaka sasa Bruno amecheza michezo 5 akifunga mabao mawili na kutoa msaada wa mabao matatu katika EPL pekee. Tangu atue United timu imenekana kubadilika kiuchezaji huku akiipa majuto Man U kwanini hawakumsajili tangu mwanzoni mwa msimu.
Zlatan Ibrahimovic – AC Milan
Baada ya kumaliza mkataba wake na LA Galaxy amerudi katika timu yake ya zamani akiwa kama mchezaji huru. Mpaka sasa amecheza michezo 11 na kufunga mabao manne. Ujio wake umeonekana kuichangamsha Milan iliyokua kama imesinzia na kupoteza nguvu yake katika Seria A huku ikiwaacha Juventus kuitawala kwa muda sasa.
Kevin Kongwe Sabato – Kagera Sugar
Kevin Kiduku mpaka sasa amefunga mabao saba akiwa amejiunga na Kagera akitokea Gwambina na kuifanya Kagera kushika nafasi ya nane akiwa na alama 41. Kwa ujio wa Sabato ambae pia ni Galacha wa mabao mwezi February kumemfanya koch Mexime kuwa na “Complete package” katika timu baada ta Kevi kua na muunganiko mzuri na kina Seseme, Mwalianzi, Ally Kagawa na Yusuph Mhilu.
Benard Morrison – Yanga sc
Ni kama Yanga walikota dodo chini ya mwarobaini kwa winga huyu wa Mghana. Ana sifa zote za kucheza kama kiungo wa pembeni na kwa uchezaji wake amefanikiwa kuongeza ubunifu katika timu akishirikiana vyema na Haruna Niyonzima pamoja na Balama Mapinduzi katika eneo la kiungo. Mpaka sasa amehusima moja kwa moja katika mabao zaidi ya 8 ya Yanga akifunga na kutoa msaada wa bao.
Hassan Kapalata- KMC
Akijiunga na KMC akitokea Mwadui fc ya Shinyanga tayari Hassan Kapalata ameweza kucheza vyema katika eneo la kiungo akishirikiana na Kenny Ally pamoja na Mohamed Samatta. Kwa uwezo wake wa kutengeneza nafasi na kuchezesha timu imepelekea KMC kushinda michezo minne mfululizo na kuendelea kujinasua kutoka mkiani.
Pamoja na sajili nzuri zilizofanywa na timu katika usajili wa dirisha dogo na baadhi ya timu lakini pia kuna sajili ambazo hazijasaidia timu kabisa na kuwapa hasara kama Yikpe wa Yanga Shiza Kichuya wa Simba na Ndikumana wa KMC.