Pamoja na kufanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Sportpesa Supercup nchini Kenya baada ya kuwafunga wababe wa Yanga Kakamega Homeboys bado usajili wao haujawasaidia.
Ikumbukwe mpaka sasa Simba hawajafanikiwa kufunga hata bao moja katika michuano hiyo baada ya kuwatoa pia kwa mikwaju ya penati Kariobangi Sharks katika mchezo wa kwanza baada ya mchezo kuisha bila bila.
Simba imefanikiwa kufika fainali ya michuano hiyo baada ya kuitoa Kakamega Homeboys kwa mikwaju ya penalti baada ya dakika 90 kumalizika bila bao kwa pande zote mbili. Katika mikwaju hiyo Simba ilipata penati zake zote huku Kakamega wakikosa penati moja, hivyo kuisogeza Simba na dimba la Goodson Park jijini Liverpool kucheza na Everton.
Katika michezo yote miwili ya michuano hiyo Simba imefanikiwa kuwatumia wachezaji wake wote wapya waliowasajili dirisha hili katika safu ya ushambilliaji, lakini hakuna hata mmoja aliefanikiwa kufunga goli.
Marcel Boniventure, Mohamed Rashidi na Adam Salamba wote walisajiliwa na Simba ili kuongeza nguvu katika nafasi ya ushambilliaji ya SimbaSc iliyokua ikiongozwa na John Bocco na Emmanuel Okwi. Wachezaji wote watatu wamefanikiwa kuitumikia klabu yao mpya lakini hakuna alieweza kutoa pasi ya bao au kufunga magoli.
Hali hii inaonyesha Emmanuel Okwi na John Bocco bado wanakazi kubwa ya kuendelea kuibeba Simba katika michuano mbalimbali katika msimu ujao.
Hueda wachezaji hawa ugeni na kutokuzoeana na wenzao kumewafanya washindwe kufanya vizuri mpaka sasa katika kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi.