Baada ya kubaki njia panda katika kufuzu robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Africa kutokana na kichapo cha mabao mawili kwa sifuri sasa uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa msemaji wake wamewaka wazi wanategemea kupata tuzo kutoka Shirikisho la mpira wa miguu barani Africa CAF.
Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo dhidi ya AS Vita Hajji Manara msemaji wa Klabu ya Simba ameonyesha shauku ya kutaka kupewa zawadi ya mashabiki bora na CAF kutokana na ushangiliaji na kujaza uwanja wa Taifa.
Hajji Manara “Hata kama tutapata matokeo mabaya (dhidi ya AS Vita) ama vyovyote itakavyokua tuzo ya mashabiki bora barani Africa itakuja Simba Sports Club “No doubt” juu ya hili. CAF wanatoaga tuzo ile kila mwaka na hakuna shaka washabiki watakaopata tuzo ni mashabiki wa Simba. ”
Manara aliongeze kua mashirikisho ya mpira yanataka viwanja vijae na Simba katika hilo hakuna shaka wanalifanya haswa.
“FIFA na CAF wanataka viwanja vijae na mashabiki wa Simba tunaongoza. Katika mchezo dhidi ya Al-Ahly mliona na pia kwenye mchezo wa JS Saoura wachezaji wao walipagawa mpaka wakaanza kupiga selfie na mashabiki manaa hawajawahi kucheza mbele ya watazamaji elfu sitini.” Hajji Manara.
Kwenye mkutano huo na waandishi wa habari Manara alizidi kusisitiza mashabiki kujaa uwanjani ili kuiwezesha Simba kuandika historia ya mpya kwa kufuzu hatua ya robo fainali.