Kwa taarifa yako tu, Juma Kaseja alianza kuichezea timu ya Taifa Tanzania mwaka 2002, mechi yake ya kwanza ikiwa katika michuano ya CECAFA dhidi ya Kenya. Tanzania ilishinda bao 1-0 (Novemba 30, 2002) pale CCM Kirumba Mwanza. Bao likifungwa na Henry Morris dakika ya 9.
Kipindi hicho stars ikiundwa na kina Athumani Machupa, Thomas Mashala, Henry Morris na Abubakar Mtiro.
Tarehe nne tena huenda akawa golini tena dhidi ya Burundi wakati tukianza kampeni ya kutafuta tiketi ya kombe la Dunia Qatar.
Wewe ulikuwa wapi 2002?