Mara baada ya leo kuandika makala kuhusu kiungo Mohamed Issa ‘Banka’ na kuhoji kwanini hayupo klabuni Yanga licha ya kusainiwa karibia miezi miwili sasa, ukweli ambao umepatikana ni kwamba mchezaji huyo wa Zanzibar amefungiwa kucheza soka kwa mwaka mmoja na Shirikisho la soka Afrika-Caf.
>>Mohamed Issa ‘Banka‘ ni usajili mwingine ‘hewa‘ Yanga baada ya Feston Kayembe?
MO Banka amefungiwa kwa kosa la kufeli kwa vipimo ambavyo viliendeshwa na Caf katika michuano ya Cecafa Kagame Cup, Novemba mwaka jana nchini Kenya ndio maana tangu wakati huo hata klabu yake iliyopita Mtibwa Sugar haikuwahi kumtumia.
Jambo la kujiuliza hapa ni kwanini TFF, ZFA kama wahusika wakuu wa soka nchini wamekaa kimya huku Yanga nao wakimsaini mchezaji aliyefeli ‘doping test’ ya Caf?