Ni mechi kali bila shaka lolote ambayo ilikuwa inawakutanisha mabingwa watetezi wa Ligi kuu pamoja na timu ambayo imepanda daraja msimu huu.
Simba kabla ya mechi hii ilikuwa inaongoza Ligi ikiwa na alama 41 wakati namungo ipo nafasi ya tano na alama 28 ikiwa na mchezo mmoja mkononi.
Namungo imeshinda mechi zote tatu za mwisho ilizocheza ugenini hivi karibuni.. Imezifunga JKT Tanzania, Mbeya City na Prisons. Na hii ndiyo sababu kubwa kwanini Namungo Leo anaweza kushinda, amekuwa akicheza vyema mechi za ugenini.
Namungo imefunga angalau bao moja katika kila mchezo kwenye mechi tano za mwisho ilizocheza kwenye VPL.. Imefunga jumla ya magoli 9 na kuruhusu 7.
Washambuliaji Reliants Lusajo na Blaise Bigirimana ndio walikuwa ni tishio zaidi katika uchambuzi wangu wa awali kwenye kikosi cha Namungo ambapo kwa pamoja msimu huu wamefunga zaidi ya magoli 10.. Pia kiungo wa kulainisha Luca Kikoti ameendelea kuwa hatari. Ni Lucas Kikoti na Blaise ndiyo wameifunga Simba mabao mawili.
Simba msimu huu haijapoteza mechi hata moja nyumbani, imepata sare mbili dhidi ya Prisons na Yanga. Kwenye mechi ambazo Simba imekuwa ikicheza nyumbani imekuwa ni mfalme haijawahi kufungwa hata mechi moja nyumbani msimu huu.
Simba imeruhusu magoli manne katika mechi tatu za mwisho za Ligi. Hii inamaanisha safu ya ulinzi ya Simba bado ina changamoto.
Hapo awali nilisema Viungo Cletous Chama, Fransis Kahata na Hassan Dilunga ndiyo wachezaji wa kuchungwa zaidi wa Simba.. Wamehusika kwa 80% ya magoli ya Simba katika michezo ya karibuni. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa katika mchezo wao wa leo dhidi ya Namungo. Kahata na Dilunga wamehusika katika magoli mawili leo, huku Kagere akifunga bao moja pia.