Jana kulikuwa na mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga , mechi ambayo ilimalizika kwa timu zote kutoka sare ya magoli 2-2 , sare ambayo ilionekana kutopokelewa vizuri na mashabiki wa Simba na mashabiki wa Yanga kuonekana kuipokea vizuri. Na moja ya lawama ambazo zinaongelewa sana ni kiwango kibovu cha Manula. Hivo tumeamua kuyaainisha madhaifu ya Manula kitaalamu.
REFLEXES
Reflexes ni hali ya golikipa kuzuia shot zinazopigwa langoni kwake iwe shot ya kichwa au mguu. Mara nyingi Haji Manula hapa huwa siyo imara sana , ni mara chache sana kwake yeye kuzuia shots zinazoelekezwa kwenye lango lake , mfano jana amepigiwa shots mbili zilizolenga goli na zote zimezaa magoli mawili.
KUHUSIKA KWENYE TRANSITION
Mara nyingi timu inapokuwa inashambuliwa na mpira ukawa kwenye Himaya ya hiyo timu. Golikipa hutakiwa kuhusika kwenye transition kwa sababu wachezaji wa timu pinzani mara nyingi huwa wanakuwa wanasogea kushambulia hivo nyuma kuna kuwa na uwazi , golikipa anatakiwa kutumia uwazi huo haraka kwa ajili ya manufaa ya timu. Hapa Aishi Manula huwa anakuwa slow sana kwenye transition.
HAENDANI NA FALSAFA YA KUCHEZA KUANZIA NYUMA
Goli la pili la jana la Simba build up ilianzia nyuma kwa mabeki , mara nyingi Simba hii imekuwa na utaratibu wa kuanzia kushambulia kutokea nyuma. Kucheza kutoka nyuma kuna faida moja , kulazimisha wapinzani wawafuate kukukaba juu , wanapokuja kukukaba juu lazima wavutike kwenda mbele na wanapovutika nyuma huacha uwazi , uwazi ambao unaweza kuwa na madhara kwao , ili timu yako iweze kucheza kwa kuanzia nyuma unatakiwa uwe na wachezaji wa nyuma ambao wanajua kupiga pasi vizuri , kuanzia kipa mpaka mabeki . Manula hayuko comfortable kwenye kuchezea mpira na kupiga pasi.