Sambaza....

Siku chache zilizopita Waziri Mwenye dhamana ya Michezo sanaa na Utamaduni nchini Tanzania Dr. Harrison Mwakyembe alitoa pendekezo la kupunguza wachezaji wa kigeni kunako ligi kuu Tanzania Bara kutoka 10 hadi watano.
Lengo la Waziri ni kuwapa nafasi ya kucheza wachezaji wa Kitanzania, na kujenga timu ya Taifa imara.

Binafsi sioni sababu ya kuwapunguza, hii ni sawa na kumpunguzia mashamba mkulima wa kipato cha chini ili alime kwenye aridhi ndogo kwa ustadi na ufasaha, (Utaleta Njaa)

Harrison Mwakyembe waziri mwenye dhamana ya michezo!

Mosi, kupunguza wachezaji wa kigeni ni kudumaza wachezaji wa ndani, ule ushindani wa kuwania namba katika vilabu vyao utapungua, Watajua na kuamini kuwa kivyovyote vile wafanye mazoezi wasifanye namba yao ipo tu.

Pili, Ligi hii itapoteza wafuasi, Mvuto na Mashabiki wengi ndani na nje ya nchi hivyo kuleta hasara kwa vilabu na shirikisho la mpira kwa ujumla.
Vuta picha ligi bila udambwi wa Morrison, bila ukabaji wa Yakubu, bila mbwembwe za golikipa ‘handsomeboy’, bila ufungaji wa kagere na Bigirimana, bila pasi za Niyonzima, hakika mengi yatapungua.

Haruna Niyonzima akimiliki mpira mbele ya Clatous Chama

Tatu, Mchezo wa mpira unataka usawa “FAIRPLAY”, muda huo huo bado tunataka wachezaji wetu wakacheze nje ya nchi ilikupata uzoefu, kwanini wa nje wasije bongo!?, Kila nchi ikitaka wachezaji wakigeni wawe watano Kina Oviedo, Dickson Job, Novatus, na wengine wenye ndoto za kwenda nje zaidi wataenda wapi?, binafsi hii si sahihi.

Nne, Nchi nyingi Duniani kote zinahitaji kuwa na ligi iliyobora na yenye ushindani ili kukuza na kuitangaza nchi kupitia mpira, na ligi haiwezi kuwa kubwa, au yenye ushidani pasi na wachezaji kutoka sehemu mbalimbali wenye uwezo mkubwa, iweje bongo tupunguze wachezaji wa kigeni?.

Mwisho, kikubwa ni wachezaji wa Tanzania kuongeza juhudi, nidhamu na uwezo wa kupambana kwa nyakati tofauti hapo ndipo soka letu litakua na si kupunguza wachezaji wa kigeni kutoka 10 hadi watano.

Sambaza....