Mwenyekiti wa bodi ya wakuregenzi ya Simba , Mohammed Dewji amedai kuwa kwa sasa wanataka kuweka mbele suala la nidhamu ndani ya timu, Tahiti huyo aliyasema hayo wakati anazungumza na kituo cha Azam Media.
Tajiri huyo amedai kuwa kwa sasa wameagiza vifaa ambavyo vitaweza kumwambia ni mchezaji yupi ambaye ni mzembe au ni mchezaji yupi ambaye anajituma.
“Nimeagiza vifaa vinakuja viko njiani , vifaa ambavyo vitakuja kugundua ni mchezaji yupi anajituma kwenye mazoezi na yupi ni mzembe. Hatutaki mchezaji mzembe”.
“Na yote haya tunafanya kwa sababu ya maandilizi ya ligi ya mabingwa barani Africa. Kwa hiyo tutajua kwenye mazoezi yupi anajituma yupi ni mzembe pia”. Alisema mwenyekiti huyo wa bodi ya Simba.
Mohammed Dewji amesisitiza kuwa ndani ya timu ya Simba hakuna mchezaji ambaye ni mkubwa kuzidi klabu. Kwa hiyo yeyote ambaye ataonesha utovu wa nidhamu hawata mvumilia.
“Ndani ya Simba hatutaki michezo michezo , tumewekeza pesa. Kwa hiyo mchezaji yeyote asiyekuwa na nidhamu hatutoweza kumvulimia ndani ya klabu ya Simba”.
“Ndiyo maana hata Bernard Morrison tulipomleta Simba kitu cha kwanza nilimwambia brother discipline. Nilimtaka aandike kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa atakuwa na nidhamu na ndicho alichokifanya”- alisema Mohammed Dewji.