Shirikisho la soka nchini Tunisia limethibitisha kumtimua kazi Kocha wa Timu ya Taifa Faouzi Benzarti baada ya siku nne tu kuisaidia timu hiyo kufuzu Kwenye michuano ya Afrika mwakani.
Katika taarifa ya Shirikisho Hilo haijaweka wazi sababu za kumtimua Kazi Benzarti lakini wamewateua makocha wasaidizi Mourad Okbi na Maher Kanzari kuwa makocha wa muda Hadi Katika mchezo wa mwezi Novemba itakapocheza na Misri.
“Bodi imeamua siku ya Jumamosi kuvunja uhusiano wetu na Kocha mkuu wa timu ya Taifa Faouzi Benzarti” taarifa ya Shirikisho hilo imesema.
Shirikisho Hilo limesema kwamba kocha mkuu mpya atatangazwa mapema mwaka 2019.
Ikumbukwe kwamba Benzarti mwenye umri wa miaka 68 alichaguliwa kuwa Kocha wa Tunisia mwezi Julai mwaka huu ikiwa ni kwa mara ya tatu kurejea kuinoa timu hiyo.
Jumanne iliyopita aliiongoza Tunisia kushinda mabao 2-1 dhidi ya Niger mjini Niamey na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Mataifa Afrika itakayofanyika mwakani nchini Cameroon.