Yanga walikuwa katika miji ya Arusha na Moshi kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya awali ya marudio dhidi ya Township Rollers ambapo ilicheza mechi mbili.
Mechi ya kwanza ilichezwa Moshi katika uwanja wa Ushirika Moshi dhidi ya Polisi Tanzania ambapo Yanga ilifungwa goli 1-0 .
Mechi ya pili ilikuwa jana dhidi ya AFC Leopards katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha ambapo Yanga ilishinda kwa goli 1-0.
Baada ya mechi ya jana dhidi ya AFC Leopards ya Kenya, kocha mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera amesema kuwa maandalizi yalikuwa mabovu na wamepoteza muda tu.
“Maandalizi yalikuwa mabovu, viwanja vilikuwa vibovu sana, tunajiandaa kucheza na Township Rollers mechi ya mipango”
“Huwezi kucheza kwenye uwanja huu kwa mpango, lazima kila mpira mchezaji apige juu abahatishe kupiga kichwa”.
“Township Rollers wana uwanja mzuri, uwanja ambao lazima tucheze kwa mpango, lazima tungecheza kwenye uwanja mzuri ili tujiandae vizuri”-alisema kocha huyo kutoka Congo.