Baada ya kutoka sare na KMC katika uwanja wa uhuru, mashabiki wa Yanga wameonesha kutoridhishwa na matokeo ya mchezo huo pamoja na maamuzi ya mwamuzi Ally Sasi.
Wakizungumza baada ya mchezo huo mashabiki hao ambao walionekana kuongea kwa ukali wamedai kuwa refa hakuchezesha vizuri ndiyo chanzo cha wao kutoka sare.
“Wanapanga kuturudisha nyuma ndiyo maana maamuzi yao ni mabovu, tulipanga tushinde back to back lakini mwamuzi katurudisha nyuma katika mchezo wa leo”.
“Nilikuwa namheshimu sana mwamuzi Ally Sasi lakini alichokifanya cha Leo amejivunjia heshima. Wachezaji wa KMC walikuwa wanafanya madhambi lakini badala ya kuwapa kadi yeye alikuwa anawaonya tu”- alidai shabiki mmoja ambaye alikuwa anazungumza na mtandao huu.
Huu ndiyo ulikuwa mchezo wa mwisho wa Yanga kwa mwaka huu kwenye ligi kuu ya Tanzania bara, mchezo utakaofuata utachezwa mwakani dhidi ya Simba ambao ni mahasimu wao wakubwa.