Inawezekana alifunga goli na inawezekana kabisa yeye ndiye aliyetoa pasi ya mwisho ya goli la Deo Kanda. Vitu viwili muhimu ambavyo Meddie Kagere alivifanya kama mshambuliaji wa eneo la Kati.
Ndivo vitu ambavyo hubeba timu na wakati mwingine ndivo vitu ambavyo humbeba mshambuliaji, hongera kwa hilo lakini swali kubwa ambalo tunatakiwa kujiuliza kwa pamoja Meddie Kagere huyu wa kuanzia mwezi wa kumi na mbili mpaka sasa ndiye yule Meddie Kagere ambaye tulizoea kumuona ?
Ni swali kubwa ambapo jibu lake linahitaji utulivu wa hali ya juu , kuna vitu ambavyo tunatakiwa tuwaze kwa pamoja. Tumuwaze Meddie Kagere ambaye alikuwa anakabia juu.
Meddie Kagere ambaye muda mwingi alikuwa hawapi nafasi mabeki wa kati kuwa na mpira tena wakiwa huru kusogea mbele kutoka katika eneo Lao na kupiga pasi.
Meddie Kagere muda mwingi alikuwa karibu na kila eneo la nyuma ambapo mpira ulikuwepo. Kiasi kwamba mabeki walikuwa hawako huru kumiliki mpira kama ambavyo walivyo huru kwa sasa.
Kasi yake imepungua , kasi ya yeye kukimbia kwa ajili ya kukabia juu (High Pressing ), kasi ya yeye kukimbia akiwa na mpira imepungua kwa kiasi kikubwa tofauti na kipindi cha nyuma kuanzia mwezi wa 11 kurudi nyuma.
Ilikuwa ngumu kuona mwezi unaisha kwa Meddie Kagere akiwa na goli moja tu. Hiki kitu ni cha kushtua , mwezi wa kumi na mbili umeisha kwa Meddie Kagere kuwa na goli moja tu. Kiwango ambacho siyo kawaida yake , ndiyo maana nikawaza ni muda sahihi kwake kuamka kabla hajaanza kupigwa maneno kama Manula