Sambaza....

Aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Yanga, David Molinga ambayo jana aliachana na timu yake hiyo amedai kuwa ni kawaida kwake yeye kuondoka Yanga kwa sababu wachezaji wengi huwa wanaondoka kwenye timu na kwenda timu zingine.

“Mimi kama mchezaji sina shida , kama Ronaldinho aliondoka Barcelona na kwenda timu nyingine siyo kitu kibaya kwangu mimi kuondoka Yanga na nitaenda timu nyingine.” Alisema David Molinga.

Kuhusu kama kweli alikuwa na msimu mbaya wakati akiwa Yanga, David Molinga amedai kuwa hadhani kama alikuwa na msimu mbaya wakati akiwa anachezea katika klabu ya Yanga.

David Molinga “Falcao”

Mimi siwezi kusema kama mambo yalikuwa mabaya Yanga.

“Nimekuwa mfungaji bora wa timu niko kwenye nafasi ya tatu au ya nne ya ufungaji bora kwenye ligi. Angalia hata Samatta ni mchezaji mzuri sana lakini kafunga goli moja tu England. Mwaka wa kwanza kwenye ligi ni kitu kigumu sana unatakiwa kuzoea ligi.

“Unatakiwa uzoee lugha , mfumo wa timu mimi nimejitahidi sana kwa mwaka wangu wa kwanza ingawa ulikuwa mgumu. Mimi nitaenda kucheza timu nyingine maisha yangu ni mpira , kabla ya kuja Yanga nilikuwa na maisha yangu mengine” alisema David Molinga.

Alipoulizwa kuhusu timu ambazo zinamtaka , David Molinga amedai kuwa miaka sasa hivi anatakiwa na timu nne kutoka Morocco , Algeria na nyumbani kwao Congo. Kwa hiyo anatazama ni sehemu ipi ambayo ni sahihi yeye kwenda.

“Kuna timu Morroco inanitaka tunazungumza nayo , nyingine iko Algeria na yenyewe inanitaka na tuko tunazungumza nayo. Hata nyumbani kwetu Congo kuna timu ambayo inanitaka kwa hiyo wakala wangu yupo anatazama ni timu gani ambayo inaweza kunifaa mimi”- alimalizia David Molinga.

Sambaza....