Baada ya Jana John Terry kutangaza kustaafu kucheza soka la ushindani baada ya kucheza kwa miaka 23. Kuna taarifa zinadai ataendelea kubaki kwenye timu yake ya Aston Villa kama kocha msaidizi.
John Terry, anatarajiwa kujiunga na Thierry Henry katika benchi la ufundi. Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal, Barcelona na timu ya taifa ya Ufaransa anatarajiwa kuwa kocha mkuu wa Aston Villa, huku John Terry akiwa kocha msaidizi.
Thierry Henry alikuwa kwenye benchi la ufundi la timu ya taifa ya Ubelgiji iliyoshiriki katika kombe la dunia la mwaka 2018 ambapo Ubelgiji ilishika nafasi ya tatu, huku Thierry Henry akiwa kama kocha msaidizi chini ya Martinez.
Hii itakuwa kwa mara ya kwanza kwa Thierry Henry kuwa kocha mkuu katika maisha yake ya ukocha. Na msimu huu aliacha kusaini kandarasi jipya na kituo cha luninga cha Sky Sports kwa ajili ya kujiingiza rasmi katika kazi ya Ukocha. Na wiki ijayo Aston Villa inatarajiwa kumtangaza rasmi kama kocha mkuu.