Sambaza....

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ Sebastien Desabre amewaita kikosini wachezaji watatu wanaocheza Ligi kuu Tanzania Bara Kwa ajili ya michezo miwili ya Kimataifa.

Desabre amewaita Nicolas Wadada wa Azam, Emmanuel Okwi na Jjuuko Murushid wote wa Simba SC katika kikosi hicho ambacho kitacheza na Cape Verde kuwania kufuzu AFCON 2019 pamoja na Nigeria katika mchezo wa Kirafiki.

Kwa mujibu wa Ratiba ya kambi timu hiyo itaingia kambini November 9 kwa kuanza na wachezaji wanaocheza Ligi ya ndani Kabla ya baadae wakina Okwi kujiunga nao.

Kikosi Kamili.
Denis Onyango (Mamelodi Sundowns), Jamal Salim (El Meriekh), Charles Lukwago (KCCA FC) and Nicholas Sebwato (Onduparaka FC), Isaac Isinde (Kirinya Jinja SS) na Murushid Juuko (Simba SC).

Wengine niTimothy Awanyi (KCCA FC), Denis Iguma (Kazma FC), Nicholas Wadada (Azam FC), Godfrey Walusimbi (Kaizer Chiefs) FC, Isaac Muleme (Haras El Hodood), Bernard Muwanga (KCCA FC), Yayo Kato Lutimba (Vipers SC), Joseph Ochaya (Lusaka Dynamo) na Hassan Wasswa (El Geish).

Pia wapo Khalid Aucho(Church Hill Brothers, India), Ibrahim Saddam Juma (KCCA FC), Tadeo Lwanga (Vipers SC), Allan Kateregga (Cape Town City), Faruku Miya (Gorica ), Ambrose Kirya (Sc Villa) na Moses Waisswa (Vipers Sc).

Pia wapo Milton Karisa (MC Oujda), Allan Kyambadde (KCCA FC), Dan Serunkuma (Vipers SC), Vianne Sekajugo (Onduparaka FC), Emma Okwi (Simba SC), Edrisa Lubega (SV Ried), Derrick Nsibambi (Smouha) na Patrick Kaddu (KCCA FC)

Sambaza....