Sambaza....

Mlinda mlango chipukizi na namba tatu wa Yanga Ramadhani Kabwili amejikuta akihitajika kushughulikiwa na kamati ya maadili ya Shirikisho la Soka nchini TFF kutokana na tuhuma alizozitoa leo katika chombo kimoja cha habari.

Kabwili amesikika akitoa tuhuma kwa klabu ya Simba ambazo  zinaashiria upangaji wa matokeo na hivyo kupeleka TFF kuhitaji ufafanuzi zaidi  kuhusiana na hilo. TFF pia imevitaka vyombo husika kufanya kazi yake katika tuhuma hiyo ya Kabwili.

Ramadhani Kabwili akiokoa hatari katika lango lake katika mchezo dhidi ya Simba sc.

Radhani Kabwili “Alinifwata kiongozi wa Simba kwa jina siwezi kumtaja akiniahidi kunipa Toyota IST ili niweze kupata kadi ya tatu ya njano ili nisiweze kucheza mchezo dhidi ya Simba. Nilikua nina kadi mbili za njano hivyo walitaka nipate kadi ya tatu ya njano katika mchezo dhidi ya JKT ili nisihusike katika mchezo unaofuata na golini akae Kindoki”

Hayo ni baadhi ya maneno aliyoyasema Kabwili alipokua akihojiwa katika kipindi cha redio.

Ramadhani Kabwili

Baada ya kauli hiyo TFF ikaamua kuipa kamati ya maadili maagizo juu ya mlinda mlango huyo kinda.

TFF ” Sekretarieti ya Tff imeiandikia kamati ya maadili kufwatilia tuhuma hizi na kujua sakata hili kiundani. TFF imekua ikipinga vitendo vyovyote vya upangaji wa matokeo katika mpira wa miguu”

Ramadhani Kabwili anatoa tuhuma hizo ni katika mchezo wa msimu uliopita katika raundi ya pili ambapo Siimba iliibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri .

Sambaza....